WAZIRI wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mkoani Ruvuma Dkt Damas Ndumbaro anaendelea kutekeleza ahadi mbalimbali ambazo ameziahidi kwenye Jimbo hilo ikiwemo ya kuwachukua baadhi ya watoto (Wanafunzi) waliohitimu darasa la saba kuwapeleka shule za Sekondari za kulipia kwa gharama za Mbunge huyo.........NA AMON MTEGA, SONGEA.
Akizungumza ofisini kwake katibu wa Mbunge huyo Joel Ndunguru amesema kuwa Mbunge Dkt Ndumbaro amekuwa akitekeleza ahadi mbalimbali za Jimbo hilo ikiwemo suala la kuwasomesha baadhi ya wanafunzi kwenye shule za Sekondari wakiwemo wanafunzi waliokuwa wakilelewa kwenye baadhi ya vituo vya watoto wenye mazingira hatarishi(YATIMA).
Katibu Joel Ndunguru amesema katika msimu huu wa mwaka 2022 Mbunge amewachukuwa wanafunzi saba(07)ambao wanne (04)wanatokea kwenye vituo vitatu vya kulelea watoto waliotokea kwenye mazingira hatalishi ,huku wanafunzi watatu(03)wanatoka kwenye familia za kawaida ambao wanawazazi wao na kuwa walipata nafasi hizo kwa kufanyishwa masahili (Interview)kadhaa na wakapata wastani uliohitajika ambapo wanafunzi wa kutokea kwenye vituo vya kulelea watoto hawajahusika kwenye masahili hayo.
Ndunguru amefafanua kuwa wanafunzi hao ambao wanne wanatokea kwenye vituo vitatu ambavyo ni St.Anithon kilichopo kata Mfaranyaki mmoja (01)St.Teresa kata ya Msamala mmoja(01) na kituo cha Swacco kata ya Mwengemshindo wanafunzi wawili (02) na wanaotokea kwenye familia za kawaida ni watatu (03)kata ya Mjini mmoja(01) kata ya Luhuwiko mmoja(01)na kata ya Ndilimalitembo mmoja(01)na kufanya jumla ya wanafunzi saba (07) wote wanatarajiwa kuanza safari yao Januari mwaka huu 2022 kuelekea Jiji la Dares-Salaam kwenye shule ya Sekondari ya Daora ambayo ni moja ya shule zinazodaiwa kufanya vizuri hapa Nchini katika suala zima la taaluma.
Amesema kuwa ofisi ya Mbunge huyo ilianza tangu misimu uliopita ya kuwachukua baadhi ya wanafunzi waliyomaliza darasa la saba kuwapeleka kwenye shule za Sekondari hasa wale wakutokea kwenye mazingira duni (YATIMA)kwa lengo la kuendeleza elimu kwa vizazi vya Jimbo hilo kwa kuzingatia usawa bila ubaguzi.
Kwa upande wake mmoja wa walezi Rosemary Haule kutoka katika kituo cha Swacco amemshukuru mbunge huyo kwa kazi ya kukubali kuwachukua watoto hao na kuwapeleka shule ya Sekondari jambo ambalo amesema linaleta faraja hata kwa walezi wa watoto hao.
Naye wa kituo cha St.Tereza Galus Mpepo amewaomba na wadau wengine waweze kujitokeza kuiga mfano wa mbunge Dkt Damas Ndumbaro kwani watoto hao wanaotokea katika mazingira hatarishi wametoka kwenye moja ya familia ambazo zipo kwenye jamii hivyo wakisaidiwa elimu watakuja kuisaidia tena jamii yetu kwa kufanya kazi mbalimbali.
Mmoja wa wanafunzi hao waliotokea kwenye vituo hivyo jina linahifadhiwa kwa sababu maalumu alishindwa kuzuia hisia zake kisha kutoa mchozi huku amesikika akisema haamini kama naye ni mmoja ambaye anaenda kusoma shule ya Sekondari ambazo wanasoma watoto wa watu wenye uwezo (Matajiri)huku akiwaomba walezi wa vituo hivyo waendelee kuwa na moyo huo huo licha ya kazi ya kulea ina misukosuko mingi.
Pia Diwani wa kata ya Ndilimalitembo Issa Chiweneke ambako kata yake imepata mwanafunzi mmoja miongoni mwa hao saba amesema kuwa Mbunge amefanya jambo kubwa na la mfano mbele ya wakazi wa Jimbo la Songea mjini hivyo amewaomba wazazi kuwasimamia watoto wao ili waweze kufanya vizuri kwenye suala zima la elimu kwa kudhibiti utolo mashuleni.
Ikumbukwe kuwa watoto (Wanafunzi)walipata nafasi hizo wakati mbunge wa Jimbo hilo Dkt Damas Ndumbaro alipotembelea vituo hivyo Disemba 26 mwaka 2021 na kutoa zawadi za sikukuu kwa watoto wa vituo hivyo kisha kuahidi kuwachukua watoto wanne kuwapeleka shule ya Sekondari ya kulipia.
0 Comments