Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Steven Kagaigai amewaagiza wakurugenzi kuhakikisha kuwa wanasimamia rasirimali fedha Kama zilivyokusudiwa katika utendaji wa kazi zilizopangwa Kwani fedha hizo zimekuwa zikija na kutowafikia watu wanoshi maeneo ya vijijini.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua mkutano wa kutambulisha mradi wa mpya wa USAID(C3HP_HIV&TB)kwa wadau mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro
Aidha amesema kuwa mara nyingi fedha zinazoletwa na wadau wa maendeleo kwa sehemu flani nyingi zimekuwa hazifiki kwa walengwa hususani waliopo maeneo ya vijijini na kusema kuwa watu wengi wa vijiji wamethoofika kwa kuwangalia kwa mucho kutokana na kitopatiwa huduma muhimu.
Amesema kuwa fedha za utekelezaji wa mradi huo unatolewa Kama msaada kutoka kwa Serikali ya watu wa marekani kwa lengo la kusaidia kupitia USAID ili kuongeza kasi ya Serikali kupambana na maambukizi mapya ya VVU ,Kifua kikuu,na upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango Kama njia mojawapo ya kukabiliana na vifo vitokanavyo na uzazi.
"Ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Serikali ya watu wa marekani na shirika la EGPAF katika jitihada zao za kupambana na maambukizi mapya ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, matunzo kwa familia zilizoathirika na janga hili la Ukimwi ,kuboresha huduma za afya pamoja na kutoa mafunzo kwa katika vituo vya huduma za afya mkoa wa kilimanjaro"Alisema Kagaigai.
Ameendelea kusema kuwa matumaini yake ni kwamba mradi huo utachangia kutatua changamoto zilizopo katika utoaji wa huduma kwenye ngazi mbalimbali katika utoaji na usimamiaji wa huduma za afya katika maeneo husika .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mradi wa USAID C3HP Kanda ya kaskazini Dr.Sajida Kimambo amesema kuwa mradi uliopita wa USAID wa boresha afya uliweza kuwafikia wagonjwa wapya elfu 93 wa kifua kikuu na waliweza kuwabaini wagonjwa wapya wa VVU na kuwaanzishia dawa ambao ni zaidi ya laki moja na elfu arobaini na Saba pamoja na kufanikiwa kufubaza makali ya HIV na kuwaingiza kwenye dawa na kutoa huduma Bora za uzazi wa mpango.
Amesema kuwa kwa mradi wa Sasa ambao ni Comprehensive client -Centered Health program,HIV and Tuberculosis (C3HP_HIV&TB).utatekelezwa katika mikoa 6 ambayo ni mikoa Ile iliyokuwa ikihudumiwa na USAID boresha afya.
Ametaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Kilimanjaro , Arusha , Manyara ,Singida ,Dodoma ,na Tabora na kusema mradi huo utakuwa wa miaka mitano huku Wanashirikiana na mashirika mengine katika kutekeleza.





0 Comments