Jamii imetakiwa kutowaficha watu wenye ulemavu kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika agosti mwaka huu ili kundi hilo liweze kujumuishwa kwenye mipango ya maendeleo ya kimataifa .mwandishi Ibrahim Kunoga MDTV Tanga
Hayo yamesemwa na Kamisaa wa Sensa ya watu na makazi mwaka 2022 Anna Makinda alipokuwa jijini Tanga na kutembelea kata ya chumba geni lengo likiwa ni kukagua vituo vya kuhesabia watu kwenye sensa ya watu na makazi ya mwaka huu.
Kamisaa Makinda alisema serekali lazima ijue kila wakati watu wake wakoje sio kuongea sana hasa kuangalia huduma za kijamii inatakiwa nchi nzima kujua taarifa zetu
Hivyo aliwataka watendaji wa mitaa na vitongoji kufanya kazi zao kwa weledi.
Alisema katika watu ambao ni muhimu kwenye sensa ni viongozi wa mtaa na vitongoji ndio watu ambao wakikataa au kugoma sensa haiwezi kufanyika.
Makinda alisema viongozi hao ndio wanajua kwenye nyumba hii kuna mtoto mlemavu kwa sababu katika nchi yetu swala la walemavu limekuwa tofauti kutokana na wengine kuwaficha ikiwa nao wana haki.
"Ulemavu huko wa tofauti wengine hawaoni, wengine wanamtindio wa akili,wengine hawawezi kutembea sasa hayo usiposema serekali haiwezi kuona lakini ni haki yake hakuna mlemavu asie na uwezo au kipaji alichopewa na mungu akifanani na cha kwetu, lakini mbona hatukukijua hicho kipaji kumbe angeweza kufanya mambo yake lakini nyie wenyeviti na watendaji mtajua kwenye hizo nyumba bila ugomvi mtakwenda kuhesabiana sisi tunawategemea kwa asilimia mia moja;Alibainisha Kamisaa Anna Makinda.
Mbali na hayo Makinda alisema lengo la serekali ni kupanga mambo kisayansi sio mbunge mmoja anasimama kupiga kelele watu wanakimbizana wanakuja kuleta kitu kumbe sio chenyewe.
Kwa hiyo la kwanza ni kuelimisha kwa wananchi kuwa tunatakwimu ambazo ni sahihi katika maeneo yetu tunayoishi
Makinda alieleza kuwa kuna zoezi la kuhesabu watu wakiwa wamelala ambapo siku Mhe, Rais bado hajaitaja lakini ni mwezi wa nane na nafikiri atataja hivi karibuni.
Alisema Hii kazi ni kazi ya kizalendo haina hela kama watu wanavyozungumza inahitaji kujitoa mno hivyo siku hiyo wanahitaji watu waliolala sio nyumbani tu ni katika jamhuri.
Kwa upande wake Msimamizi Maandalizi ya sensa mkoa Wa Tanga Tumaini Komba amesema zoezi limeenda vizuri na wanaendelea vizuri kwani kwa sasa anawachora ramani ishirini na mbili na kwa siku wana uhakika wa kumaliza mitaa ishirini na moja.
Tumaini aliendelea kwa kusema kuwa kwa mitaa yote mia moja sabini na moja ndani ya siku tisa wanakuwa wameshamaliza hivyo wanategemea kupata ushirikiano kutoka mkoa wa Kilimanjaro hivyo wakija wanaweza kumaliza mapema ili ifikapo mwezi wa pili wawe wameshakamilisha.
0 Comments