Na,Jusline Marco:Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Said Mtanda amekabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi 413 wanaotoka katika familia zenye uhitaji ambao wamechaguliwa kujiunga na shule mbalimbali za sekondari katika jiji la Arusha.
Akikabidhi vifaa hivyo katika hafla ya kukabidhi mahitaji ya Shule kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza iliyofanyika katika shule ya sekondari Naura Halmashauri ya jiji la Arusha,Mtanda amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote wanaripoti shuleni kwa wakati.
"Baada ya siku kadhaa kupitia Mamlaka zetu tutaanza sasa kusimamia sheria ya kuhakikisha wale ambao hawajawapeleka watoto shule wanawapeleka shule kwakutumia mkondo wa serikali kwasababu muda wa mapumziko umekwisha sasa tunachohitaji ni watoto wote waliofaulu waende darasani na wale walioandikishwa darasa la kwanza waende darasani."Alisistiza Mtanda
Aidha Mtanda amelipongeza jiji la Arusha kwa kuandaa motisha kwa walimu ambao masomo yao yamefanya vizuri ambapo amewataka kuendelea kuutekeleza mpango huo kwani walimu ndio wanaofanya kazi kubwa katika ufundishaji na kupelekea Mkoa kuongoza katika sekta ya elimu kitaifa mara kwa mara.
"Wakuu wote washule nina wapongezeni sana na walimu wote ninatambua uwepo wenu na sisi serikali tutasimama nanyi kuhakikisha kwanza zile changamoto ndogondogo zinazowakabili ambazo nyingine zinasababishwa na baadhi ya watu tuweze kuzirekebisha ili mambo yaweze kwenda vizuri.Alisema Mkuu huyo wa Wilaya
Sambamba na hayo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa kazi anayoifanya na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwake ambapo amewataka watumishi wote wa serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mbunge huyo na kwa Meya na madiwani wote wa jiji la Arusha ili kuweza kuyimiza azma ya serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi.
"Muda wa masuala ya maneno maneno na mambo ya fitna hayana maana kwani uchaguzi ulishakwisha sasa ni wakati wa kuchapa kazi,kwahiyo ndugu zangu wananchi tushirikiane kwa ajili ya maendeleo ya Arusha.
Naye Meya wa Jiji la Arusha Maxmilian Iraqhe katika hafla hiyo amesema lengo la jiji la Arusha ni kupandisha kiwango cha ufaulu hadi kufikia asilimia 100 ambapo kwa kidato cha nne kwa mwaka jana walikuwa na ufaulu wa asilimia 87.5 na kwa mwaka huu wamepansa hadi kufikia ufaulu wa asilimia 92.5 huku ufaulu wa juu walioufikia kwa mwaka jana kwa kidato cha sita ni asilimia 99 lengo ni kuhakikisha ufaulu huo kuupeleka mpaka asilimia 100.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arusha Mrisho Gambo pamoja na mchango wake ndani ya jamii ameahidi kutoa daftari 500 kwa wanafunzi pamoja na taulo za kike kwa wanafunzi wa kike 50 kwa kipindi cha miezi 6 ambapo pia ametoa fedha zilizotengwa kwa ujenzi wa madarasa na hazikutumika kutokana na serikali kutoa fedha za ujenzi huo,fedha hizo zielekezwe kwenye ukarabati wa madarasa kwenye shule mbalimbali.
Naye Afisa elimu Mkoa wa Arusha Abel Ntupwa amesema kama Mkoa bado wanandoto kubwa kutokana na juhudi zinazofanywa za kuwasaidia na kuwainua wengine ambao wanahitaji msaada,mkoa umedhamiria kufuta daraja 0 kwa mitihani ya kidato cha nne kuanzia mwaka huu.
0 Comments