Header Ads Widget

MAHAKIMU WAKAZI WA MAHAKAMA YA MWANZO WATAKIWA KUBADILISHA MAHAKAMA HIZO KUWA BORA





Jaji Mkuu Mstaafu Mhe, Mohammed Chande Athumani amewataka mahakimu  wakazi wa mahakama ya mwanzo kubadilisha mahakama hizo ziwe bora ili wananchi wapate haki zaidi na kwa haraka



Mhe  Chande ameyasema hayo kwenye mafunzo elekezi ya mahakimu wakazi wapya 35 yenye lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa mahakama wakiwemo mahakimu ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa weredi na ufanisi na kwa kiwango ambacho mahakama ya Tanzania inahitaji kwenda mbele..




Mafunzo hayo yamefanyika katika chuo cha uongozi wa mahakama IJA wilayani lushoto Alisema watanzania wanahaki ya kutendewa haki na mahakimu wenye kisomo cha sheria.



Alisema mahakama ya mwanzo taswira yake imebadilika na changamoto yao ni kuendelea kuibadilisha ili iwe bora zaidi na wananchi wapate haki kwa haraka zaidi.




Jaji Chande aliendelea kusema kuwa zaidi ya 75% ya kesi ya kesi ambazo ziko mahakamani ziko mahakama ya mwanzo na nyie mahakimu wa mahakama ya mwanzo ndio taswira katika kuhakikisha mnatenda haki kwa wananchi.



"Mnakwenda kwenye mahakama ambayo ndio nguzo ya mahakimu utendaji bora, utendeji mbovu, malalamiko vyote hivyo ni mahakama ya mwanzo kwa wingi wake sababu nyie ndio nguzo ya mahakama kwa mategemeo ya viongozi wenu na wananchi hivyo hakikisheni mnajenga rekodi safi ya mahakama  za mwanzo ;Alibainisha Jaji Mohammed Chande.



Kwa upande wake Msajili wa Mahakama kuu ya Tanzania Mhe, Sharmillah Sarwate ameeleza kuwa  mahakimu wakazi hao wapya 35 wamepelekea idadi kuongezeka ambapo kwa sasa wana jumla ya mahakimu wakazi 1359.



Alisema Mahakama ya Tanzania kupitia mkakati ambao unatekelezwa chini ya mradi wa maboresho imefanya maboresho mengi sana ikiwemo  kuelekeza katika rasirimali watu.



Amebainisha kuwa matumaini ya mahakama ya Tanzania kwamba mafunzo hayo hayataishia kwenye makaratasi Bali yatakuwa endelevu kwa ajili ya kuwawezesha kufanya vizuri wao kama watu, lakini pia kuiwezesha taasisi na nchi kwa ujumla na kutekeleza jukumu lake lililopo katika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya ibara ya 107.



Nae mkuu wa chuo cha uongozi wa mahakama IJA Mhe, Dkt Paul Kihwelo anaamini mahakimu hao watakuwa ni chachu chachu kubwa na hawatamuangusha kwa kwa kiapo ambacho wamekiapa.



Mhe, Kihwelo alisema ataendelea kuwajenga ili wakifika katika sehemu zao za kazi wakafanye kazi na kutekeleza kile ambacho uongozi wa mahakama wanataka, na kile ambacho watanzania wanataka 




Mahakama imewaamini kwamba mnastahili kwenda ya pili hivyo kitu ambacho mnatakiwa kujenga ukweli ni nyie kubadilika.


"Kuna baadhi ya maeneo yalikuwa ni changamoto lakini kwa sasa mahakama imebadilika zamani kesi ilikuwa haziendi lakini kwa sasa kasi ya kwenda mashauri iko juu sana mawakili wanalalamika kwamba inakwenda spidi sana;Alisema Mhe, Paul Kihwelo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI