Header Ads Widget

EWURA YATOA ELIMU JUU YA SHERIA NA KANUNI MPYA KUHUSU NISHATI YA UMEME

 




Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA) kanda ya kaskazini imetoa elimu juu ya sheria na kanuni mpya kuhusu nishati ya umeme kwa wadau mbali mbali wakiwemo wanafunzi wanaosoma fani ya umeme katika vyuo mbalimbali vya ufundi vilivyopo kanda ya kaskazini sambamba na mameneja wa shirika la umeme(TANESCO)............Na Gift Mongi_ Moshi Kilimanjaro



Kutolewa kwa elimu hiyo kutawawezesha wanafunzi watakaohitimu katika vyuo hivyo kujua sheria na taratibu za kufuata ili kufanya kazi ya ufundi wa umeme kwa weledi na kuachana na mafundi wa mitaani(vishoka)wasio na sifa.



Mhandisi Lorivi Long'idu ni meneja wa kanda ya kaskazini (EWURA)ambapo alisema mamlaka hiyo kwa sasa ipo katika mpango maalumu wa kukutana na wadau wote wa umeme kwa kanda ya kaskazini na lengo ni kuongeza uelewa wa sheria na kanuni mbalimbali .


Alisema hadi sasa tayari makundi kadhaa wameshakutana nayo ikiwemo wanafunzi wa fani ya umeme kwenye vyuo mbalimbali vya ufundi kwa kanda ya kaskazini sambamba na mameneja wa kanda ya kaskazini wa shirika la umeme nchini(TANESCO).


"Hii ni zoezi endelevu na ni jukumu letu kutoa elimu hiyo kwa  vijana hususan

waliopo kwenye vyuo kwani ndio nguvu kazi ambao wanatarajia kuingia

kwenye ajira kwa siku za karibuni hivyo ni vyema kuanza kuwandaa mapema" alisema



Damiani Mawole alisema kupitia Elimu ambayo EWURA waliyoitoa tayari imewabadilisha kifikra na kujua haki wajibu na sheria mbalimbali za matumizi ya nishati hiyo muhimu kwenye maisha ya kila siku tofauti na ilivyokuwa kwa kipindi cha nyuma,


“Elimu kama unavyojua haina mwisho lakini kila siku tunaendelea kuelimishwa hususani kuhusu hizi sheria mpya lakini pia njia sahihi ya kupata leseni ili kufanya kazi za umeme naona ina maana sana”alisema



Alisema tayari elimu inayoendelea kutolewa imeweza kuwasaidia na tayari wana uelewa nayo tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma jambo lililopelekea kazi ya ufungaji umeme kuwa ngumu.



"Mfano ni kuwa leseni daraja A hutolewa ili kufanya kazi za umeme katika msongo wa aina zote isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”" anasema



Kwa mujibu wa Mawole ambaye ni fundi umeme mkongwe alisema  leseni daraja B nayo hutolewa ili kufanya kazi za umeme mpaka msongo wa kati (33,000V) isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.



Daraja C hutolewa ili kufanya kazi za umeme mpaka msongo wa chini (400V) isipokuwa kazi zilizoruhusiwa chini ya daraja “S1, S2 na S3”.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI