Header Ads Widget

CCM MKOA WA IRINGA WAMPINGA JOB NDUGAI

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Kimetaka wanachama na Viongozi  mbali mbali ndani ya mkoa huo kuacha kutoa matamko yanayovuruga jitihada za Serikali iliyopo madarakani na kuwa hawatawavulimia wote watakaobainika .

Kuwa chama kina taratibu zake kutumia vikao rasmi na sio kutumia vyombo vya habari kutoa matamko yasiyo na Afya ndani ya chama na Serikali  iliyopo madarakani .

Akitoa tamko la CCM mkoa wa Iringa Kwa wanahabari leo Katibu mwenezi CCM mkoa wa Iringa Hilary Kipingi alisema wao kama chama mkoa hawajapendezwa na Kauli iliyotolewa na Spika wa Bunge Job Ndugai ya kupinga jitihada za Serikali kukopa mikopo ya kuendesha miradi .

Alisema Kauli ya Ndugai imelenga   kumkwamisha  Rais Samia Suluhu Hassan  katika  kuliletea Taifa maendeleo kuwa  wao kama  chama mkoa wanapongeza jitihada za Rais Samia Katika kuendelea kutafuta fedha za kuliletea Taifa maendeleo .

Kuwa  mikopo  ni sehemu ya maendeleo na  hata nchi kubwa zimekopa mikopo kama hiyo .

Kipingi alisema kuwa  mbali ya kazi kubwa inayofanywa na Rais  samia katika    ujenzi wa miradi mbali mbali  wapo  baadhi ya  viongozi wanaibuka na kupinga .


Alisema kuwa  tangu   Rais Samia aingie madarakani  mwezi  machi mwaka  2021  kumekuwepo na  jitihada  kubwa  zenye mageuzi makubwa katika  Taifa  na maendeleo makubwa  kwa  kuwepo kwa mambo makubwa ambayo yamefanyika kwa kipindi  cha miezi tisa  aliyokuwepo madarakani   na  kila  mmoja ni shahidi kwa kazi  hiyo.

“Deni  la taifa  linakaribia  shilingi Tirioni 70  Lakini  tutambue  kuwa deni  la serikali ya  awamu ya  sita  imekuwa  ni serikali  yenye uwazi  zamani ya kwanza  hadi  ya tano  fedha  zilikuwa  zikikopwa  lakini  uwazi  ulikuwa hauwekwi  wazi  wala wananchi  mlikuwa hamuelezwi  serikali  imekopa  nini na imefanyia  nini lakini Mheshimiwa  Samia  amechukua  fedha  Trilioni moja  na  bilioni miatatu  fedha ambazo baada ya  kuzipata  ameshirikisha  bunge  na  viongozi wa  serikali  pamoja na kufanya kikao  kueleza matumizi ya  fedha  hizo  watanzania  wote  waliona  na  hili jambo la  mfano na la kupongezwa “  alisema  Kihongosi

Kuwa  iwapo  kiongozi  mkuu wa nchi anaweza  kuchukua  fedha na kuainisha  matumizi yake  kwa  mwananchi  anajua  wazi kuwa  fedha  iliyokopwa inakwenda  kufanya nini .

Alisema  faida ya  mikopo  huo  ni kuwa hakuna riba  yoyote kwa  serikali na  ni  deni litakalolipwa kwa zaidi ya miaka  20  tena  pasipo  riba  yoyote  ile na  fedha  hizo  zimesambazwa  kwenye ujenzi  wa  vyumba  vya madarasa na  sekta ya afya  ,maji  na maeneo mengine kila mkoa.

Pia  alisema  fedha  hizo  zimeelekezwa  kwenye  uboreshaji wa  miundo mbinu ya  barabara kila kona ya  nchi  hii .

Aidha  alisema kwa  kipindi  kifupi cha  serikali ya  wamu  ya  sita madarakani  fursa  nyingi  zimekuwepo  kila  eneo  ambapo kwa  vijana  wa  vyuo  vikuu  kwenye  kipindi  cha  serikali  hii  ndipo  walipopata  mikopo  zaidi  kuliko  wakati  mwingine wote kwa  mikopo zaidi ya  bilioni 570  .

Alisema  kuwa  kwa  miradi  inayoendelea  nchini  ni  miradi  itakayonufaisha vijana  wengi  zaidi na  wao kama  vijana  hawatakubali  kuona  kuna   viongozi  wanatumia vyombo  vya habari  kutaka  kumkwamisha Rais kwa  kumsema  vibaya kwa  viongozi hao kabla ya hawajafanikisha  kumkwamisha  Rais  watakwamishwa  wao maana  yeyote anayesimama na kumpinga Rais  kwao ataonekana ni adui ni lazima ashughulikiwe .

“  Iwapo  wewe  ni kiongozi  ndani ya  nchi  hii  ama  kiongozi ndani ya  chama  una  hoja  ya  kumshauri  Rais  ni  vema  kutumia  vikao husika  kufikisha  ushauri  wako  kuliko  kwenda  kwenye  vyombo  vya habari ama  kutumia majukwaa  ya nje  kumsema  vibaya  kiongozi huyo hatavumiliwa hata kigodo .alisema Kipingi 






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI