Header Ads Widget

WAZIRI MWAMBE - WAZAZI SHIRIKISHENI WATOTO WENU, BENKI FUATENI BIDHAA MPYA NBC

 


Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji Goffrey Mwambe amewataka wazazi kuwashirikisha watoto wao katika masuala ya Uendeshaji wa kampuni wanazozimiliki Ili kusaidia kampuni hizo kuendelea kuwepo pindi muazilishili akiwa amestaafu ama amefariki.


Agizo hilo amelitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la tatu la local content liliandaliwa na baraza la uwezeshaji kiuchumi (NEEC) linalofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa maktaba mpya uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo amesema kampuni nyingi zinakufa pindi muazilishi anaposhindwa kuendelea na kazi hiyo.




"Makampuni makubwa yote duniani yanaendeshwa na familia, wanarisishana na yanafanya vizuri, wazazi tuwe na utaratibu wa kufanya kazi na watoto wetu, tuwaajiri Ili tuwatengeneze kuwa wakurugenzi wa baadae"amesema Waziri Mwambe.


Aidha, ameyataka Mabenki yote nchini Tanzania kufuata bidhaa mpya iliyotolewa na Benki ya ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kumpatia mteja mkopo kutokana na mkataba wake, kwani kazi kubwa ya Benki ni kupokea na Amana na kutoa mikopo.


Hata hivyo, amewataka waandaji wa kongamano hilo kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wamiliki wa kampuni, mabenki,Sekta binafsi pamoja wanafunzi wa vyuo Ili waweze kujadili kwa pamoja masuala ya local content ambapo hii itawasaidia kuwajengea uwezo wanafunzi kuweza kujiajiri na kuondokana na dhana ya kuajiriwa.



Amesema kuwa, katika suala la kuweka akiba kwa nchi ya Tanzania bado lipo nyuma sana, hivyo amelitaka baraza la uwezeshaji kiuchumi kufanya juhudi za kuendeleza watu wa ndani sanjari na kuwaalika watu wa nje wenye mitaji mikubwa.


"Naomba Benki zetu ziwe za kisasa tuimarishe mifumo yetu, tuwe wabunifu katika huduma tunazozitoa na sio kusubiri mteja aliyeshindwa kulipa deni kwenda kumfilisi"amesema Waziri Mwambe.


Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji kiuchumi (NEEC),  Beng'i Issa amesema kuwa, kongamano hilo linatoa fursa kwa watanzania kukuza uchumi jumuishi pamoja na kushiriki katika miradi mbalimbali ya Kimkakati na utekelezaji wake .


Aidha, amesema utekelezaji wa local content nchi Tanzania umelenga kutoa ajira kwa watanzania, zabuni katika kampuni za kitanzania ikiwemo bidhaa wanazozalisha, mafunzo na uanzishwaji wa Teknolojia pamoja na kuinua mfumo wa miradi.



Hata hivyo, amesema pia linapanua ukuaji wa uchumi wa nchi ya Tanzania pamoja na kupanua wigo wa ajira kwa watanzania pamoja na kupunguza umaskini wa kipato.


Ameongeza kuwa, Local content imelenga kuzalisha ajira kwa wingi hususani kwa vijana ambapo ajira elfu 52 zimeshazalishwa nchini Tanzania kutokana na program ya local content ambapo asilimia 70 ni vijana kati ya umri wa miaka 20 mpaka 35.


Naye, Mkurugenzi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Dr Frederick Ringo amesema kuwa, kwa kutambua mahitaji na  changamoto wanazopitia wajasiriamali wa Tanzania, kupitia dhana ya local content Benki hiyo imekuja na suluhu ya changamoto zao.


"Miongoni mwa changamoto wanazopitia wajasiriamali ni dhamana hasa kwa wafanyabiashara wadogo, hivyo NBC tumekuja na suluhu ambapo mteja hatohitaji  tena kuwa na dhamana, mkataba alionao tu utamuwezesha kupata mkopo"amesema Ringo


Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Heri James amesema kwa niaba ya viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya kukamilika kwa kongamano hilo, wao  walioserikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi pamoja ma wananchi watayachukua yote yanayotokana na kongamano hilo kama dira, mwelekeo na Usimamizi wa ushirikishwaji wa wananchi katika kuhakikisha dhamira hiyo iliyozungumzwa inakwenda kutoa uhalisia kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI