Mkuu wa idara ya Benki wa kiislam (KCB) Amour Muro amesema benki hiyo imejipanga vizuri kutoa huduma za kifedha Ili kuhakikisha kila mtanzania anapata fedha kirahisi ili aweze kutimiza ndoto zake.........Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati alipokua katika Mkutano wa 21 wa wanachama wa TPSF na kongamano la Biashara na Uwekezaji katika ukumbi wa maktaba mpya kutoka chuo kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM).
Aidha, amesema kuwa, Benki hiyo ina matawi zaidi ya 13 huku wakiwa na mpango wa kuongeza mengine Ili kuweza kutoa huduma hiyo nchi nzima.
Hata hivyo, amesema benki hiyo, imewawezesha watu wengi zaidi sana kupitia program zao za tujiajiri ambapo wanufaika kwa mwaka uliopota walikua 500 lakini kwa mwaka huu wamefikia 900 huku washirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo veta .
"Tumekua tukiwawezesha watu hususani vijana kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35 kwa njia ya kuwawezesha kibiashara, kielimu na kifedha, hii ni kuwasaidia vijana kuweza kutimiza ndoto zao"amesema Muro.
Hata hivyo, amesema wamejikita pia kutoa huduma kidigital ambapo inamuwezesha mteja kupata huduma za kibenki kwenye simu, computer,bila hata kufika tawini ama kwa wakala.
0 Comments