Header Ads Widget

WATATU WAUAWA KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI MKOANI KAGERA.

 




Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limewauwa watu watatu wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi  waliokuwa wamejiandaa kwa utekaji wa magari katika eneo la Nyabugombe, Kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo......Na, Titus Mwombeki- MTDTV BUKOBA.


Tukio hilo limebainishwa na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani humo Awadhi Jumaa, na amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Decemba mosi mwaka huu majira ya saa nane na kuthitisha kuwa jeshi Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa wapo watu wapatao saba wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameonekana katika milima ya Nyabugombe wakiwa wamevaa makoti marefu ndipo Polisi wakaweka mtego na kuwasimamisha kwa ajili ya kuwahoji ndipo  watu hao walianza kujibizana kwa risasi.



“Askari wetu walirushiana risasi na watu hao wapatao saba na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu ambao walifariki wakati wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitli  teule ya Biharamulo huku wengine  walifanikiwa kuroka kabla hawajakamatwa, askali wetu waliendelea kufanya upekuzi ambapo walifanikiwa kukuta silaha moja aina ya AK 47 iliyofutika namba na magazine mbili zikiwa na risasi 51 na kitambulisho kimoja cha Burundi chenye jina la Coyitungiye Venancie mkwilima wa Muyinga Burundi”


Kamanda Jumaa amesema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali teule ya Biharamulo kwa uchunguzi wa madakitari .



” Msako mkali bado unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata majambazi wengine waliotoroka ili kukomesha vitendo hivyo vya uhalifu,”amesema Jumaa.


Aidha,amewaomba wananchi wa mkoani Kagera kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi Katika kuripoti matukio mbalimbali yanayoonekana kuleta uvujifu wa amani mkoani humo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI