Header Ads Widget

WANANCHI WATAKIWA KUTOKOMEZA UNYWAJI WA POMBE HARAMU

Mbunge wa rombo mkoani Kilimanjaro ambaye pia ni waziri wa kilimo nchini prof.Adolf Mkenda amewataka wananchi kupambana na kuhakikisha kuwa unywaji wapombe haramu unatokomezwa .Mwandishi  Rehema Abraham MDTV ,Kilimanjaro


Amesema kuwa swala la unywaji wa Pombo  haramu ni tatizo la Tanzania mzima na lipo katika nchi nzima na kwamba halihusisnia na wilaya moja pekee .


Amesema hayo wakati alipokuwa mkoani Kilimanjaro katika katika kikao cha kamati ya ushauri mkoa,(RCC) , kilichokua na lengo la kujadili maendeleo na namna na kupatia ufumbuzi changamoto zilizopo latika utendaji kazi wa mkoa .


Amesema kuwa" pombe Kama  banana zingine Zina kibali kutoka TBS lakini zilivyopelekwa huko kupimwa zinaonekana hazina viwango ,na naamini kinachotokea ni kwamba TBS wakishapima na kuthibitisha Ile pombe watengenezaji wakati mwingine wanapuuza vile vigezo walizopewa wanatengeneza kwa namna nyingine ,kwa sababu suala la kutoa kibali ,ni suala la kufanya sampling ambapo unaangalia inavyotengeneza na Kupewa kibali kwa hiyo tutawahimiza sana TBS wawe wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara"Alisema Mkenda.


Ameendelea kusema kuwa Jambo la muhimu ni kwahimiza watu wawe wanakunywa pombe bàada ya kazi Kama ambavyo watu wengi wanafanya .


Katika hatua nyingine amesema kuwa pamoja na unywa wa pombe watu wa rombo wanachapa kazi kwa kujitolea katika shughuli mbalimbali za maendeleo Kama kujitokeza katika ujenzi wa Madaraja na ujenzi wa madarasa za fedha za uviko 19.


Sanjari na hayo amesema kuwa wilaya ya rombo imepongezwa kwa kuwa ya kwaza katika kumaliza mapema ujenzi wa madarasa 44 ya utekelezaji wa mradi  ya uviko19 ambapo amesema kumalizika mapema kwa madarasa hayo ni kutokana na wananchi kujitokeza kwa wingi kusaidia ujenzi huo.


Amesema kuwa kutokana na wananchi kujitolea kwa wingi kwa wananchi na pia Mkuu wa wilaya hiyo ya rombo Kanal Hamisi Maiga amesaidia katika usimamizi mzuri .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI