Mbunge wa jimbo la Sengerema mkoani Mwanza Khamis Tabasamu amenyanyuka na kumkataa (kumchomea utambi) Meneja wa Wakala wa barabara wilaya hiyo, Clemence Kihinga kwa kudai Meneja huyo amekuwa akishindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Tabasamu ametamka wazi kuwa, wabunge wa majimbo ya Sengerema na Buchosa hawamtaki meneja huyo kwa kuwa amekuwa ni kibuli na amekuwa akikwamisha shughuli za maendeleo.
Tabasamu ametoa kauli hiyo leo Desemba 19 mwaka 2021 wakati wa kikao cha barabara (road board) kilichokuwa kikiendeshwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel.





0 Comments