Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Sengerema Khamis Tabasamu amewaomba wananchi wake kuendelea kumuunga mkono Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali jimboni humo ikiwemo maji,afya barabara,elimu n.k.
Aidha amewataka wananchi kuchangamkia fursa zitakazopatika katika mgodi mpya wa Sotta Mining ambao unatarajiwa kuanza kufanya uzalishaji baada ya miezi 18,kauli hiyo ameitoa katika mkutano wa hadhara uliohudhukiwa na wakazi wa kata sita wa kueleza utekelezaji wa ubunge wake kwa kipindi cha 2021.





0 Comments