Header Ads Widget

WAITARA NDANI YA STENDI YA MAGUFULI GHAFLA KUHUSU NAULI

           


NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amefanya ziara ya kushitukiza kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli jijini Dar es salaam na kubaini vitendo vya ulanguzi wa tiketi kwa abiria.Mwandishi Frederick Siwale - Mdtv Dar es salaam.


Mhe,Mwita Waitara alifika mapema Mbezi kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli ili kufuatilia hali ya utoaji huduma kwa watoa huduma za ukataji tiketi kwa abiria na kukutana na madudu kinzani na taratibu na miongozo ya usafirishaji abiria.         


Akiwa katika gari la kampuni ya Najmunisa lenye namba za usajili T.606 DDR  ya kutoka Dar es salaam kwenda Bunda alibaini abiria nauli wamelipishwa sh.100,000 badala ya sh.60,000 na kuamru abiria wote warudishiwe fedha zao zilizozidishiwa na safari iendelee.                  



" Haiwezekani kabisa kipindi chochote achilia mbali kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa mtoa huduma za usafirishaji kuamua kupandisha nauli mamlaka zitamshughulikia tu" Alisema Mhe.Waitara.   


Alionekana kucharuka na kuwa mbogo kufuatia vitendo vya unyanyasaji wa abiria vinavyofanywa na watu wachache kuamua kuwapandishia nauli abiria .                                


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi alilazimika kuingia pia katika basi la kampuni ya AN     LABOR CLASSIC la kutoka Dar es salaam kwenda mkoani Tabora kujiridhisha na kuona hali halisi ndani ya basi hilo na kisha kuendelea na ukaguzi wa kushitukiza ndani ya mabasi .                        


Upande wake mkuu wa Oparesheni Mafunzo na elimu haki za abiria Taifa wa Taasisi ya kutetea haki za abiria ( CHAKUA) Bw.Wilson Damo alisema kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka mara nyingi watoa huduma za usafiri ndiyo huibuka na vitendo vya kufanya ulanguzi wa bei za tiketi na kuomba mamlaka nyingine zisimame na kushirikiana kwa pamoja kuwapigania abiria wasidhurumiwe.                


Bw.Damo akiwa stendi ya Magufuli akiongoza timi ya CHAKUA kutoa elimu na kutetea abiria kupitia kipaza sauti aliwataka abiria kutokubali kunyanyasika mahali popote Nchini wawapo safarini na kuwataka wafunguke .    


"Abiria CHAKUA tupo Nchi nzima ,Polisi wa kikosi cha usalama barabarani na LATRA wapo Nchi nzima ya Tanzania toeni taarifa za uvunjifu wa haki za abiria badala ya kugeuzwa kuwa shamba la bibi" Alisema Damo.                  





Katika Oparesheni hiyo ya kushitukiza katika stendi ya mabasi yaendayo mikoani ya Magufuli pamoja na Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Waitara ,LATRA walikuwepo wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji Bw.Giliad Ngewe,CHAKUA na Askari wa kikosi cha usalama barabarani .          


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI