Header Ads Widget

SERIKALI YAOMBWA KUTAMBUA MCHANGO WA USHIRIKA WA KIMTANDAO

 


SERIKALI imeombwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Ushirika wa kimtandao na kutoa leseni lengo likiwa ni kupambana na umasikini katika jamii zilizopo pembezoni hasa maeneo ya  vijijini ili kuweza kupata huduma za kimtandao......Na Hamida Ramadhan Dodoma



Akiongea mara baada ya kumalizika kwa Warsha ya siku mbili jijini Dodoma Sophia Mumba mshiriki kutoka Wilaya ya Kondoa amesema ushirika huo umewasaidia kupunguza umasikini kwani wajasiriamali wakulima wafugaji na watu wote wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji wameweza kutangaza biashara zao kupitia mtandao.


Kadharika amesema ushirika huo wa kimtandao umeweza kusaidia kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto kwani tangu kupatikana kwa mtandao  wa intaneti wamewasaidia kupata taarifa za msingi ambapo gari la kubebea wagonjwa imekuwa sio shida kwa tena kwao.


"Kiliochetu tunaomba serikali itusikie na itutambue sisi ni wadau kama wadau wengine na tunania nzuri ya kuwasaidia wao serikali ili kupambana na kuondoa changamoto zilizopo katika jamii watupatie lesseni waweze kufanya kazi zetu za kusimika minara tayari tuko na bizaa lakini hatujapewa kibali na mamalaka ya mawasiliano TCRA," amesema Sophia 



Naye Enyaso Mtei kutoka mkoa wa Kilimanjaro mshiriki wa mafunzo hayo amesema wamejifunza kuhusu mtandao na namna ya kwenda kuwasaidia watu waliopo pembezoni ambao wanashida ya mtandao na sasa wanakwenda kuwasaidi kupata mtandao kwa bei na fuu na kwa haraka iliwaweze kulahisisha shughuli zao za kimaendeleo.


Kwa upande wake Mhandisi Stella Manyanya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kufunga kwa mafunzo hayo amesema Kongamano hilo hufanyika mara moja kwa mwaka huku alieleza lengo kuu la mafunzo hayo likiwa ni kusogeza karibu huduma ya mtandao na kuwafikia watu mbalimbali waliopo vijijini. 



Amesema jamii ilizoea kusikia ushirika wa mazao na sasa umekuja ushirika wa mtandao ambao unaonyesha wazi utasaidia watu kutumia nguvu nyingi na kazi kuendelea kwa haraka. 


"Changamoto kubwa katika taifa letu ni pamoja na sera za huduma  za mawasiliano kupitia mawimbi ya Television kumekuwepo na vikwazo kwani sera za ugawaji wa masafa imekuwa ikiwatenga wadau wengine.


Aidha amesema ni ukweli usiopingika gharama za mtandao zipo juu huku akisema  jambo hilo linatakiwa kufuatiliwa na sera zilizopitwa na wakati zibadilishwe.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI