Header Ads Widget

SERIKALI MKOA WA IRINGA YATAKA JITIHADA ZA BTI KUUNGWA MKONO

  

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Moyo wa pili kulia waliokaa akiwa na Viongozi wa taasisi  isiyo  ya  kiserikali ya  Brand Tanzania Initiative(BTI) Leo  baada ya kufunga mafunzo ya siku tatu jana mjini Iringa kushoto kwake ni Mlezi wa BTI balozi mstaafu  wa Madagascar Balozi Rajab Omar Luhwavi

SERIKALI  ya  mkoa  wa  Iringa  imetaka jitihada zilizoanzishwa na   taasisi  isiyo  ya  kiserikali ya  Brand Tanzania Initiative(BTI) kwa   kutangaza fursa  za  utalii  ndani ya  mkoa  wa Iringa na Tanzania  kuungwa  mkono   zaidi  kwani  zinashabiana na mkakati  wa  Rais  Samia Suluhu  Hassan wa kutangaza  utalii wa Tanzania ulimwenguni kupitia The  Royal  Tour.

Mkuu  wa  mkoa wa Iringa  Queen Sendiga ametoa Rai   hiyo  Leo katika  ukumbi  wa Iringa Sunset  wakati  akifunga  mafunzo ya siku  tatau  kwa watendakazi wa  taasisi ya BTI , alisema  kuwa lengo la serikali  ya  awamu ya  sita  ni  kuona sekta ya  utalii inatangazwa zaidi  duniani Ulimwenguni kupitia  sekta  hiyo  serikali  inakuza  uchumi  wake kwa  watalii  zaidi  kuja  kutalii nchini.

Mkuu  wa  mkoa  ambae  aliwakilishwa na mkuu wa  wilaya ya  Iringa Mohamed  Moyo  alisema  kuwa  kuwa  moja kati ya maeneo  ambayo yanaweza  kuvutia  watalii  wengi  zaidi  kutembelea  vivutio  vya  utalii ndani ya  mkoa wa Iringa ni pamoja na uboreshaji wa  miundo  mbinu ya viwanja  vya ndege  kazi  ambazo kwa  mkoa  wa Iringa  imeendelea kufanyika kwa  uwanja  wa  ndege Nduli  kuboreshwa na  ifikapo  mwezi macha    mwakani  uwanja  huo  utaanza kutumika .

Pia  alisema  serikali  ina mpango  wa  kuweka  kituo  cha  utalii  eneo la  Kihesa  Kilolo  ambacho  wakati  wowote  kituo  hicho  kitaanza  kujengwa kwani  mipango  yote  ipo   tayari  .

Aidha  alisema  ipo  miradi  ya uendelezaji  wa  utalii  mikoa ya kusini (REGROW)  inaendelea  kazi  ikiwa ni pamoja  na  kusogeza  umeme katika  hifadhi ya  taifa ya  Ruaha  pamoja na  kuboresha  barabara ya  kuelekea hifadhi ya  Ruaha kwa  kiwango  cha  lami.

Alisema  jitihada  zinazofanywa na BTI zinakwenda  sambamba na  jitihada  za  Rais Samia kupitia filamu  aliyoirekodi ya The  Royal  Tour  hivyo  alisema  kama  serikali ya  mkoa wa  Iringa haitakubali  kuona  kuna  mtu anakwamisha   jitihada za BTI  katika  kutekeleza majukumu  yake ya kutangaza  fursa  za  utalii ndani ya  mkoa  huo  na  fursa  nyingine .

Hivyo  alisema  kupitia  maboresho ya  uwanja  huo ni  rahisi kwa  watalii  zaidi  kuendelea   kufika  kutalii katika  vivutio  vya utalii  ndani ya mkoa  wa  Iringa na mikoa ya  nyanda za  juu kusini  hasa  ukizingatia  mkoa  wa Iringa ni lango  la utalii kwa  mikoa ya kusini mwa  Tanzania.

Katibu  mtendaji  wa  BTI Lusekelo Mwandemange   alisema  kuwa   taasisi  hiyo  yenye miaka  9  sasa  lengo  lake kuu ni kuitangaza  nchi  kimkakati  pamoja na kujenga  ushindani  wa  nchi .

Alisema  taasisi  hiyo  inaundwa na  vijana  kutoka  nchi  nzima   na  kuwa kazi yao  kubwa  kufanya uchambuzi  kitaifa  na kimataifa , kuisaidia  nchi kusonga  mbele  kimaendeleo   pamoja na  kufanya  tathimini ya  mambo  mbali mbali  kwa  kuhusisha  wataalamu  mbali mbali .

Akijibu swali  la  wanahabari  kuhusu kauli   tata  zinazotolewa na baadhi ya  viongozi nchini ambazo  zinaonesha  wazi ninavuruga  Taifa , alisema  pamoja  na  kuwa asingependa  kujibia nani kasema nini  na nani kajibu  nini  ila  kun a shida  ya baadhi ya  viongozi kupima mambo ya  kutoa  kwa umma  jambo ambalo  ni baya  sana .

Hivyo  wao kama  BTI   wanaendelea  kuwajengea  uwezo  viongozi na  vijana  nchini  ili  kujua  nini  nchi  itataka na  kitu gani  ambacho  si kizuri  kwa Taifa .

Katibu  huyo  alisema tayari  BTI  wamekwisha andika  maandiko  kadhaa na kuyapeleka  Ikulu  wakati wa Serikali ya  awamu ya nne  chini ya  Rais Jakaya  Kikwete  na  kuwa  wanampango  wa  andiko  hilo kumpelekea Rais  Samia Suluhu  Hassan.

Mwandemange alisema  kupitia tafiti  mbali mbali  ambazo BTI  imefanya  zimeweza  kuzaa matunda na kutolea mfano juu ya tafiti ya matumizi ya  dawa  za  kulevya  kwa  vijana  kuwa  wakati  walipofanya  utafiti  wao Tanzania  ilikuwa na taswira  mbaya sana na  matumizi ya  dawa za kulevya  na  wakati  huo  kuna  vijana  zaidi  800  walikamatwa  china na vijana  zaidi ya 400 walikamatwa  Afrika  ya  kusini ila  kwa sasa  taswira   hiyo  imepungua  sana.













Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI