Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameelekeza kila Halmashauri kuwalipa fedha wakandarasi wa usafi kwa wakati na kutoa mikataba ya muda mrefu Ili waweze kufanya kazi zao kwa wakati na kuondokana na visingizio vya kutozoa taka.MwandishibFatma Ally MDTV Dar es Salaam
Agizo hilo amelitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na wakandarasi wa usafi jiji hilo, ikiwa ni hatua ya kuelekea uzinduzi wa kampeni ya usafi unaotarajiwa kufanyika Dec 4 mwaka huu ambapo kimkoa itafanyika kata ya Kivukoni.
Aidha ameelekeza Halmashauri hizo kuanza kutoa mikataba ya muda mrefu kwa kampuni za Usafi tofauti na Sasa ambapo wanatoa mkataba wa mwaka mmoja jambo linalopunguza ufanisi.
Hata hivyo, amewataka wakandarasi wa Usafi kuhakikisha wanatekeleza jukumu la kimkataba kwa kufanya Usafi na kuajiri Vijana Wenye uwezo wa kazi tofauti na Sasa ambapo baadhi wameajiri Wazee wa miaka zaidi ya 60.
Aidha, amemtaka kila Mkandarasi kuwa na namba ya simu Mkurugenzi wa Manispaa husika na kutoa taarifa pindi wanapobaini machinga wamerudi kwenye maeneo yaliyokatazwa na kuwazuia kutekeleza majukumu yao ya Usafi.
Hata hivyo, ameitoa wito kwa Wananchi kuunga mkono Kampeni hiyo kwa kufanya Usafi wa Kaya na Usafi wa kila Jumamos ya mwisho wa Mwezi.
Kwa upande wao Wakandarasi wa Usafi kutoka Manispaa za Mkoa huo wamemuahidi RC Makalla kuwa wamejipanga kuhakikisha mandhari Jijini inakuwa katika Hali ya Usafi huku wakieleza kukerwa na tabia ya baadhi ya Wanasiasa wanaojiingiza kwenye kamupni za Usafi.
0 Comments