Header Ads Widget

NASHAURI KADA ZA CHINI WAPEWA KIPAUMBELE CHA WAJUMBE WA MABARAZA YA WAFANYAKAZI" -DED KAYANDABILA.

 





Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Ndg. Elias M. Kayandabila ameshauri kuwapa vipaumbele na kuwashirikisha wafanyakazi wa kada za chini kwenye mabaraza ya wafanyakazi....


 Aliyasema hayo katika mkutano wa baraza la wafanyakazi lililokutana kwa kwa ajili ya kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwaka 2020/2021 uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Muleba.


Akizungumza katika Mkutano huo Ndg. Kayandabila amesema kuwa inaleta maana sana kuwa na watu wa kada za chini kabisa kwenye baraza la wafanyakazi kwa sababu ndipo mahala pao pekee wanaweza kuja kusema matatizo yao.



"Watu wa kada za chini wakipata nafasi kama hizi ambazo tuko huru kuongea juu ya changamoto zetu za kiutumishi anaongea jambo ambalo liko kwenye moyo wake sasa kwa viongozi ambao ni wasikivu huwa wanafarijika sana kukutana na wale watu. Kwahiyo ningeomba pia wakati mwingine tusikae tu sisi wakubwa na watu wale wa chini waje watuambie matatizo yao" alimesema  Kayandabila.


Katika Mkutano huo changamoto mbalimbali zimewasilishwa na wajumbe wa mkutano huo yakiwemo masuala ya malipo ya likizo kwa watumishi, upandishwaji wa vyeo, malipo ya wastaafu, malipo ya ugonjwa na masuala ya kujiendeleza kitaaluma.




Kwa upande wake  Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Ndg. Charles Ntaki akijibu juu ya suala la wajumbe kuhusu idadi ya walimu waliopanda vyeo amesema kuwa walimu 1,633 wamepanda vyeo na walimu 44 wamebadilishwa kada. 


Lakini pia ameongeza kwa kusema kuwa mikakati ya kutoa motisha kwa watumishi kila mwaka tarehe 1 mwezi wa Mei kila sekta huwa inatenga kiasi kisichopungua Tsh. 300,000/= kwa ajili ya mfanyakazi bora aliyefanya kazi kwa uadilifu, uaminifu, kukidhi matakwa ya kisheria ya kujaza fomu ya mapitio ya utendaji kazi ya wazi kikamilifu na kufanya kazi kwa ubora kila mwaka. Kupitia vyama vya kiutumishi huwa anapewa motisha ya kuwa mtumishi bora.


Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya Muleba Masatu Chisumo amesema kuwa kwa upande wa wastaafu hakuna mstaafu ambaye anadai kwa maana ya gharama za kusafirisha mizigo mara baada ya kustaafu na kuhusu suala la uhamisho  amesema kuwa walimu wamekuwa wakilipwa kadri fedha zinavyopatikana.


Naye Afisa Elimu Msingi Mwalimu Seveline Philipo Msyangi ameeleza kuwa suala la kujiendeleza kitaaluma ni la mtu mmojammoja na mtu huyo ndiye anaomba kwamba anataka kwenda kusoma bila kuathiri msingi wa mafunzo na wamekuwa wakiruhusiwa.



Naye Afisa Mifugo na Uvuvi Ndg. Emmanuel Masha amevishauri vyama vya wafanyakazi kusimamia maslahi ya watumishi kwani wamekuwa wakikatwa fedha kwenye mishahara pasipo kuona manufaa ya vyama hivyo.


Mwisho wajumbe wa mkutano huo wamemshukuru Mkurugenzi Mtendaji ambaye ndiye Mwenyekiti wa Baraza hilo kwa kufanya mkutano huo ambao hapo awali mkutano kama huo haukuwahi kufanyika.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI