Header Ads Widget

JESHI LA UHAMIAJI MKOA WA KILIMANJARO LAENDELEA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA MAENEO YA MIPAKANI

 


Jeshi la uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro limesema kuwa linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo ya mipakani hususani kwenye maeneo ya rombo na Mwanga,na baadhi ya maeneo ya wilaya Siha ili kuhakikisha kuwa mkoa unakuwa salama na wahamiaji hawaingii kinyume Cha Sheria ya nchi.


Amesema Afisa   uhamiaji  msaidizi  wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Eduard martin wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofsini kwake mkoani Kilimanjaro.


Aidha amesema kuwa wamekuwa wakiendelea kutoa elimu katika maeneo hayo ya mpakani na maeneo mengine yenye mikusanyiko ya watu juu ya wananchi hao kuwa walinzi wa mipaka kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi kuhakikisha kwamba wahamiaji haramu hawaingii nchini.


"Kwa hiyo tumekuwa na mafanikio kwani tumeweza kukamata baadhi ya watu mfano tulikamata raiya wanne wa somalia waliokuwa na hati ya bandia ya nchi ya Kenya wakiwa na msafirishaji raiya wa Kenya mwenye asili ya kisomali , ambao tuliwakamata maeneo ya wilaya ya same na mpaka Sasa tumeshawafikisha mahakamani kwa kosa la kuingia Nchi bila kibali.Alisema Martin.


Hata hivyo Amesema kuwa mkoa wa Kilimanjaro upo salama na vyombo vya ulinzi na usalama havilali kwani vinaendelea kufanya doria na kaguzi mbalimbali kuhakikisha kwamba hakuna wahamiaji haramu na hawaingii Katika mkoa .


"Nitoe wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa ili kuhakikisha kwamba raiya wote wa kigeni ambao hawafuati Sheria tunawafikia na kuwachukulia hatua"Alisema Martin.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI