Header Ads Widget

M/KITI JUMUIYA YA WAZAZI PWANI AMPONGEZA RAIS SAMIA



Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi mkoa wa Pwani Jackson Kituka amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa vyumba vya madarasa vinavyoendelea kujengwa katika mkoa mzima wa Pwani kwa fedha za mkopo kutoka benki ya dunia IFM lengo likiwa ni kumaliza kabisa tatizo la upngufu wa vyumba vya madarasa katika kila mwaka nchini.


Amesema hayo kwenye mkutano wa Kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya Wazazi mkoa wa Pwani wakati ikuzungumza na wanachama wa jumuiya hiyo Kata ya Mkuza Kibaha Mkoani Pwani.



Alisema kila mwaka mkoa umekuwa ukihangaika na tatizo la upngufu wa vyumba vya madarasa kwa darasa la kwanza na kidato cha kwanza lakini mwaka huu kero hiyo haipo tena katika mkoa mzima.


Kituka alisema safari za Rais Samia nje ya nchi ndio zimeletea taifa matunda hayo ya vyumba vya madarasa nchi nzima.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI