Mbunge viti maalum mkoa wa Pwani Subira Mgalu amemkabidhi kuku 2600 Mwenyekiti wa Jukwaa la Kuimarisha Wanawake kiuchumi mkoa wa Pwani Mariamu Ulega kwaajili ya Kugawa kwenye vikundi 17 vya Wanawake wa wilaya ya Mkuranga katika mkutano wa jukwaa la wanawake Wilaya ya Mkuranga kwa ufadhiri wa wizara ya mifugo na uvuvi ili wakafuge kwa lengo la kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais Samia la kuwasimamisha kina mama kiuchumi.
Awali akifungua Mkutano huo wa Jukwaa hilo la Wanawake Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Khadija Nassri Ally aliwataka wanawake hao kutumia fursa ya kuanzisha viwanda vitakavyowakwamua kiuchumi kwa kutumia fursa la uwekezaji mbalimbali uliopo katika mkoa huo wa Pwani.
Mwenyekiti wa jukwaa hilo la Wanawake mkoa wa Pwani Mariamu Ulega ameshukuru kwa msaada huo wa kuku kutoka wizara ya mifugo na uvuvi kwa kusema wasichoke kuwasaidia maana wataomba tena kuku kwa ajili ya wilaya zilizobaki katika mkoa wa Pwani.
0 Comments