Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) ameongoza kikao cha wataalam kutoka Wizara ya Kilimo pamoja na wawekezaji wa kampuni ya Tree Global ambapo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw. Gregory Hess ameelezea jinsi ya matumizi ya Teknologia katika ukuzaji wa mimea.
Mkutano huo una lengo la kuingia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni hiyo katika upandaji wa miti ya korosho na Cocoa kwa lengo la kutunza mazingira na kupunguza umasikini, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ndogo za Wizara, Kilimo IV leo jijini Dodoma.
0 Comments