Header Ads Widget

MGOMBEA UBUNGE WA ACT NGORONGORO AAHIDI NEEMA

Mgombea ubunge wa jimbo la Ngorongoro kupitia chama  cha ACT wazalendo Johnson Mahuma   amesema.  endapo wananchi wa jimbo hilo watampa ridhaa ya kuliongoza Jimbo Hilo atapeleka kilio cha changamoto ya barabara inayotoka mto wa mbu kuelekea Loliondo ambayo ndio kilio kikubwa kwa wananchi wa Tarafa ya Loliondo. mwandishi Pamela Mollel MDTV  Ngorongoro


Akizindua Kampeni za kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya ubunge kwa jimbo la ngorongoro mgombea ubunge kwa  chama cha ACT Wazalendo Johnson Mahuma anasema kilio kikubwa kwa wakazi wa jimbo hilo ni Barabara inayotoka mto wa mbu kuelekea Loliondo na endapo atapata ridhaa atapeleka changamoto hiyo bungeni



Mahuma amesema kilio Cha wananchi kutokana na ubovu  wa barabara hiyo kina zaidi ya miaka 60 Hali inayosababisha wakazi wa Loliondo kufata bidhaa nchi jirani ya Kenya hivyo kujengwa kwa barabara hiyo kutawafanya wananchi kupata bidhaa za kiurahisi tofauti na ilivyo Sasa


"Ukiangalia kwa Sasa kuliko mwananchi wa hapa akachukue bidhaa Arusha Yuko radhi aende nchi jirani ya Kenya, Sasa mkinichagua nitapambana na hii changamoto"Alifafanua.


Aidha Mahuma Alifafanua kuwa Ngorongoro ni miongoni mwa majimbo yanayokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo,migogoro ya Mara kwa Mara,maji,pamoja na mazingira magumu ya watoto kupata elimu


Awali wananchi wa Tarafa ya Loliondo wakimuuliza maswali mgombea  huyo walitaka kujua endapo mgombea  atawezaje kuzitatua changamoto nyingi zinazolikabili jimbo hilo ikiwemo migogoro ya mara kwa mara ambayo watangulizi walishindwa kuitatua


"Hebu tuambie wewe utawezaje Kutatua migogoro inayotukabili au ndo unataka kura tukishakuchagua utuache uende mjini"?Aliuliza Saruni Losioky mkazi wa Loliondo.


Akijibu changamoto hizo Mgombea huyo akawataka wananchi kumpa uwakilishi ili kufikisha kilio chao bungeni  na kwamba changamoto hizo zitatatuliwa endapo wananchi watakubali kufanya mabadiliko


"Tusiishi kwa kukariri Mimi sitakuwa Kama viongozi waliopita nijaribuni kwa kunipa kura muone nitakatoyafanya"Aliongeza Mahuma.


Jimbo la ngorongoro linafanya uchaguzi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Willium Tate Olenasha mbapo mpaka sasa tayari vyama  sita tayari vimekwishachukua form za kuomba ridhaa ya uwakilishi katika Jimbo Hilo

Miongoni mwa vyama ambavyo mpaka Sasa vimekwishazindua kampeni ni pamoja na CCM,ACT Wazalendo, NLD,UDP,SAU, na  NRA  tayari kwa maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika  Dec.11 mwaka huu


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS