Msanii wa kizazi kipya mkoani Morogro Gervas Keula maarufu Kaka STREVO Kushiriki na wadau wengine wameanzisha kampen malum ya kusaidia watu wenye mahitaji maalum inayofahamika Kama TWENZETU NA BUKU
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro STREVO amesema kuwa watu maarufu ikiwemo Wasanii wananafasi kubwa katika kusadia jamii hivyo yeye kushirikia na wadau wa maendeleo wameona vyema kutumia umaarufu wao katika kusaidia jamii.
Strevo anasema mkoani Morogoro Kuna vituo vingi vya watu wenye uhitaji ikiwemo yatima ,walemavu hivyo program hiyo itakua endelevu na kuleta tija
"hii programu hataishia hapa lazima na kwakuanzia sikukuu ya Christmas tunaenda kupelekea taulo za kike ,sabuni,Nyembe na nguo za ndani kwa wafungwa wanawake waliopo gerezani mkoani hapa"STREVO
Kwa upande wake mmoja wa Wadau hao akiwemo Ahmad Machaku ametoa wito kwa jamii Kushiriki katika programu hiyo
Machaku anasema kuwa badala ya watu maarufu kutumia umaarufu wao katika vitu visivyo vya maadili na kupata skendo na Kiki ambazo hazina manufaa ni vizuri wakaungana pamoja.
"lengo la zoezi hili ni kusaidia jamii hivyo kwa wale wenye uwezo wanaweza kununua vifaa moja kwa moja na wengine kutuma kiasi chochote kwa kuwasiliana na uongozi ili lengo letu litimie"Machaku.





0 Comments