Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI PROFESA PATRICK NDAKIDEMI AONGEA NA VIONGOZI WA UWT KUTOKA KATA ZA HALMASHAURI YA MOSHI

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro Prof. Patrick Ndakidemi amewashukuru wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania kutoka CCM (UWT) wilaya ya Moshi vijijini kwa juhudi zao za kukipigania chama na kuhakikisha kinashinda katika uchaguzi mkuu wa 2020.


Kikao hicho cha baraza kilichowajumuisha viongozi Mwenyekiti na Katibu wa Wilaya UWT, na Wenyeviti na Makatibu wa Kata UWT kutoka Jimbo la Moshi Vijijini (kata 16) na Vunjo (kata 16) kilifanya katika ukumbi wa ccm wilaya ya moshi vijijini.



"Wakinana mlifanya kazi kubwa ya kukipigania chama chetu kuhakikisha tunashinda katika nafasi ya Urais, Ubunge na Madiwani niwapongeze sana ninyi ni jeshi kubwa na mkiamua kitu kinatokea" alisema Prof. Ndakidemi.


Aliwaomba viongozi hao wawe mabalozi kwenye kuelezea uma kazi nzuri za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali yao ya CCM iliyoko madarakani ambayo wameipigania.



Mbunge huyo alisema kuwa, serikali imefanya mambo makubwa ya maendeleo hivyo ni jukumu la kila mwanaccm kuyasemea ili wananchi watambue nini kilichofanyika ili ifikapo 2025 katika uchaguzi mkuu uwe mwepesi kwa chama.


Aidha aliwaasa akina mama wajiunge kwenye vikundi ili iwe rahisi kupata huduma ya mikopo kutoka halmashauri na taasisi nyingine za fedha.


Kwa niaba ya akina mama waliokuwa ukumbini, Mwenyekiti wa UWT Kata ya Uru Kusini alimshukuru Mbunge kwa kuja kuwashukuru, na kuahidi kumpa ushirikiano yeye na Madiwani na viongozi wengine wa Chama na Serikali kwenye kuleta maendeleo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI