Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI PROFESA PATRICK NDAKIDEMI ASHIRIKI MBIO ZA MR UK MARATHON MJINI MOSHI



NA WILLIUM PAUL,MOSHI.

 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo na Mbunge wa Babati Mjini Mheshimiwa Pauline Gekul na Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro Profesa Patrick Ndakidemi  wameshiriki katika mbio za Mr UK Marathon zilizofanyika mjini Moshi ambazo zilianza na kuishia MOSHI CLUB. 


Viongozi hao waliambatana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kilimanjaro na washiriki mbalimbali kutoka maeneo ya Tanzania. 



Mratibu wa mbio hizo Profil Massawe kutoka Dar es Salaam ameeleza kuwa mbio hizo zimeshirikisha zaidi ya wakimbiaji mia tisa zililenga kukusanya fedha za kukarabati kitengo cha wagonjwa Mahututi katika Hospitali ya Mkoa Mawenzi, Kilimanjaro. 



Alisema kwamba, ameridhika na mashindano haya yaliyofanyika kwa mara ya kwanza Kilimanjaro, na kudai kuwa yatakuwa endelevu.


Mbio hizo zilihusisha ushindani katika uendeshaji wa baiskeli kilomita 50, kukimbia kilomita 5, 10 na 21. 



Mbunge  Prof. Patrick Ndakidemi alishiriki mbio za kilomita 5 na kumaliza vizuri na kukabidhiwa Medali.


Mratibu wa Mashindano hayo ndugu Profil  Massawe alikabidhi hundi ya shilingi milioni kumi kwa hospitali ya rufaa ya Mawenzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI