UONGOZI wa Klabu ya Mbeya road fc ( Watoto wa Nyumbani Makambako) Mkoani Njombe wameamua kuja kivingine...........Na Frederick Siwale- Mdtv Njombe.
Katika kikao cha tathimini baada ya kutwaa ubingwa wa mkoa wa Njombe ,kilichofanyika desemba 17 mwaka 2021 Viongozi hao wamedai timu ya Mbeya road fc ni timu ya Wananchi wa Makambako hivyo wataikabidhi kwa Wana Makambako.
Katika kikao hicho cha tathimini Kocha wa Mbeya road fc Albet Gama alisema timu ilicheza ikiwa inakabiliwa na changamoto ya kifedha na kuwashukuru wadau wote waliojitolea michango yao kuisaidia Mbeya road fc hadi kufikia hatua ya kuongoza kituo cha Makambako na kuvuka hatua ya nane bora kule Tandala Ikonda Wilayani Makete ambako ubingwa ulichukuliwa.
Gama alisema shukrani zake ni kwa Wadau wa soka katika halmashauri ya Mji Makambako wakubwa na wadogo .
Mwenyekiti wa Mbeya road fc Musa Mwaipopo alisema kwa hatua hii iliyofikiwa umefika wakati ambao Uongozi unapaswa kuunda bodi ya Wakurugenzi na udhamini ili kuingia vizuri katika michuano ya Mabingwa wa mikoa inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwaka 2022.
Mwaipopo alisema umoja na mshikamano vikiwepo kati ya Uongozi na Wadau wa Mbeya road uwezekano wa kufanya vizuri upo na kusonga mbele .
" Wajumbe timu hii isingeweza kupata ubingwa wa mkoa wa Njombe katika kipindi cha Mwaka 2021/2022 pasipo nguvu na michango ya Wanamakambako" Alisema Mwaipopo.
Upande wake Katibu mkuu wa Mbeya road fc Godfrey Mwakasita alisema pasipo umoja na Wadau kuichangia klabu kwa kikubwa na kidogo ikiwepo ni pamoja na michango ya fedha, Jezi ,mipira na vyakula ingekuwa vigumu kuchukua ubingwa wa mkoa.
" Thubutu yake kuna Wadau hapa bila wao isingewezekana kufanya miujiza ya kidgitali kuzichakaza timu kadhaa na nyingine zilichapwa katika viwanja vya nyumbani kwao ni funzo kwetu" Alisema Mwakasita.
Wajumbe Mohamed Kamara na Mohamed Kilimbe kwa Upande wao walisema baada ya ubingwa ali imekuwa kubwa na kurudi kuwaangukia wadau wa Soka Makambako kuiona Mbeya road fc kuwa ni timu yao na hivyo kuomba umoja na mshikamano viwe dira na ufunguo wa kufanya vizuri katika michuano ya Mabingwa wa mikoa.
Hata hivyo wajumbe wa kamati ya Mbeya road fc katika kikao hicho walipendekeza kuundwa kwa kamati kubwa mbili za kuhakikisha kuwa Mbeya road inafanya vizuri kuanzia ngazi hii ya mkoa , Mabingwa wa mikoa, daraja la pili,daraja la kwanza hadi ligi kuu inawezekana .





1 Comments
God bless my team🙏🙏
ReplyDelete