Header Ads Widget

MAMENEJA WA TANESCO KANDA YA KASKAZINI WAPIGWA MSASA

 




Ili kuhakikisha kunakuwepo na uhakika wa ukuaji wa kiuchumi wenye uhakika ni lazima kuwepo kwa mazingira ya uhakika ya upatikanaji wa nishati ya umeme........Na Gift Mongi




Ni ukweli usio na mashaka ndani yake kuwa shughuli zilizo nyingi za uingizaji kipato zinategemea sana nishati ya umeme katika maeneo yaliyo mengi na ndio maana serikali imekuwa ikitilia mkazo kwa wananchi kuunganishiwa nishati hiyo.



Hata hiyo bado zipo baadhi ya changamoto ambazo bado kimsingi zimekuwa zikiikabili sekta hii ya nishati ambayo ipo chini ya shirika la TANESCO na kushindwa kufikia malengo yake ambapo jitihada zimeendelea kuchukuliwa ili kuondokana na kadhia hiyo.



Baadhi ya changamoto hizo ambazo zimeonekana kulikabili shirika hilo la umeme ni  wizi wa umeme, uharibifu wa miundombinu, ukatikaji wa umeme, ukuaji mdogo wa mapato ya Shirika, upotevu wa umeme na matatizo ya utoaji wa huduma ikiwemo uchelewaji katika kutatua matatizo ya dharura yanayowakabili wananchi.



Mamlaka ya usimamizi wa nishati na maji (EWURA)imekuwa ikichukua hatua mbali mbali katika kuhakikisha kunakuwepo na maboresho ya nishati hiyo muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini.



Hatua hizo ni pamoja na kuweza kuwajengea uwezo viongozi wa shirika la umeme (TANESCO)ikienda sambamba na kuwakumbisha kanuni mbalimbali katika utekelezaji wao wa majukumu ya kila siku.



Kwa upande wa kanda Kanda ya Kaskazini(Manyara,Tanga,Arusha na Kilimanjaro)kumeendelea kufanyika jitihada za utolewaji wa elimu kwa viongozi wa Tanesco ambapo zoezi hili kinaendeleshwa na EWURA lengo likiwa ni kuleta mabadiliko na kuendenadana na hali ya uhitaji wa nishati hiyo.


Mameneja  waandamizi wa Tanesco pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo Kanda ya Kaskazini wamepewa elimu  na kuelimishwa kanuni na taratibu za ufanywaji wa kazi ili kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali ya awamu ya sita yanatimia na kazi za umeme zinafanywa kwa kuzingatia kanuni na Sheria.



 Meneja wa mamlaka ya usimamizi wa nishati na maji(EWURA)  Kanda ya kaskazini Lorivi Long'idu amesema kuwa  elimu inayoendelea kutolewa  kwa wadau hao itasaidia  kumaliza changamoto zilizopo na kuboresha zaidi huduma kama ilivyo dhamira kuu ya serikali



"Sisi kama wadhibiti tunafanya kazi mbalimbali katika kufanya kaguzi zetu ambazo tunakagua miundombinu ya Tanesco, ufanyaji kazi wa Tanesco,kwa hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja hivi tulikuwa tulifanya kaguzi mbalimbali na tumekutana na baadhi ya changamoto ambazo tumeona ni vyema tukakumbushana wajibu wa kila upande yaani Tanesco na sisi kama msimamizi"Alisema Lorivi.



Katika hatua nyingine amesema kuwa wanawaelimisha ili wajue mdhibiti amepewa jukumu hilo kwa mujibu wa Sheria na wanawajibika kwa mdhibiti katika kutoa taarifa kwa kufanya kazi zao kwa kufuata misingi ya ufanyaji wa kazi wa maswala mazima ya umeme.



Hata hivyo amesema kuwa changamoto zilizopo ni utoaji mbaya wa huduma kwa wateja  hivyo elimu hiyo itasadia kuondoa changamoto hizo na kuboresha huduma ambapo pia itaweza kwenda kuwafikia wananchi walio wengi.



Anasema katika sekta hiyo ambayo inaonekana kuwa tegemezi kwa ukuaji wa uchumi ni lazima kuwepo na kukumbishana wajibu na mabadiliko ya sheria nankanuni mbalimbali ili kuweza kuondoa urasimu usio na ulazima hali ambayo itaenda kuleta matokeo chanya.



"Hizi changamoto za utoaji wa huduma zisizoridhisha ni lazima mkae chini mjitafakari kuwa mteja ama mlaji anatendewa haki?na Kama hapana ni kwanini na ninwapi pakurekebisha ili Sasa tuweze kupiga hatua mbele zaidi ya hapa tulipo"anasema



Kwa mujibu wa meneja huyo ni kuwa kumekuwepo na malalamiko ya Mara kwa Mara kutoka kwa wateja Kuhusiana na huduma zisizoridhisha ama zipo chini ya kiwango na kuwa baada ya kupewa mafunzo yakukumbushwa wajibu kadhia hiyo itaenda kumalizika kwa kipindi kifupi



"Malalamiko yapo na ndio maana sis(EWURA)Kama msimamizi tukaona tukae ili kuweza kuona ni wapi mlikwama lengo ni kuhakikisha mlaji(mteja)anafurahia upatikanaji wa huduma  na sio tena  kero kwa upande wake na sidhani kama hilo pia ndio lengo la serikali yetu hii"anasema



Mhandisi Evarist Simon ni mkaguzi mkuu wa umeme wa EWURA nchini amesema semina kwa wadau hao muhimu inajikita zaidi kujadili na kutatua changamoto na mapungufu yaliyopo katika utolewaji wa huduma za nishati kwa wananchi na kuboresha zaidi huduma hiyo.



Amesema kuwa katika Semina hiyo wamelenga maeneo matatu kwenye upande wa ufundi na upande wa kanuni ambazo Ewura wanazitunga kutoka kwenye Sheria mama ya mwaka 2018 ya umeme .



Akizungumza kuhusiana na mapungufu yaliyopo kwenye utolewaji wa huduma za TANESCO kaimu meneja Kanda ya Kaskazini mhandisi Charles Urio anasema kuwa kutaenda kufanyiwa kazi kwa mapungufu yaliyoonekana  sambamba na kuwataka   wananchi kuzingatia sheria katika matumizi ya huduma.



"Wananchi sasa nao wakumbuke nao wanna wajibu mkubwa katika kusimamia na kuzingatia sheria za matumizi ya huduma lengo likiwa ni kila mwananchi kutambua sheria inasemaje ili asilalamike kabla ya kujua muongozo uliopo"anasema



Diwani wa kata ya Katangara Mrere wilayani Rombo Venance Mallel anasema bado kunahitajika semina elekezi hususan kwa shirika hilo ili kupeleka huduma stahiki kwa wananchi walio wengi.



"Hawa tunawategemea Sana ila naona ipohaja wakumbushwe wajibu wao wa mara kwa Mara kwani Kuna kipindi wanaishi Kama vile wamejisahau katika kuwahudumia wanachi hususan kwa wakazi waliopo maeneo ya pembezoni.



Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI