Header Ads Widget

MADEREVA WANAOENDELEA KUBETI WAONYWA ARUSHA

 



Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha


Kuelekea Msimu huu wa sikukuu za x mass na mwaka Mpya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia kikosi cha usalama Barabarani kimefanya ukaguzi wa zaidi ya magari mia moja(100) na kutoa elimu kwa madereva na abiria wanaotumia vyombo vya moto kwenda mikoa mbalimbali hapa Nchini.


Akiongea na madereva hao Leo December 18.2021 katika stand Kuu ya mabasi yaendayo mikoani mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP Solomoni Mwangamilo amewaonya baadhi ya madereva wanaoendelea kuendesha magari kwa mwendokasi kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya mdereva kubashiri (BET) ili kuwahi kufika wanakokwenda amewaonya kuacha mara moja tabia hiyo.



Aidha, amewasihi wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za madereva wanaokiuka sheria za usalama Barabarani na kwenda mwendokasi ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika 


Sambamba na hilo emeendelea kusisitiza madereva kufuata sheria na taratibu zilizowekwa ili kupunguza ajali hasa kipindi hiki ambacho kuna wingi wa magari barabarani.



Pia abiri wanaotumia vyombo hivyo wamelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha hususani Kikosi cha usalama Barabarani kwa kuwa na utaratibu wa mara kwa mara kukagua vyombo vya moto hasa kipindi hiki ambacho wamiliki wengi hutumia fulsa ya sikukuu za mwisho wa Mwaka kulejesha magari yao Barabarani.



Nao baadhi ya madereva wamelishukuru Kikosi Cha usalama Barabarani kwa kutoa elimu ya mara kwa mara kwa madereva na abiria ili kuweka uelewa wa pamoja ili kuepusha ajali zisizo za lazima Barabarani.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI