WATOTO yatima wa kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi katika Manispa ya Iringa wapewa faraja ya sikukuu ya Chrismas kwa kuandaliwa chakula cha pamoja na uongozi wa kituo hicho .
Akizungumza mara baada ya chakula hicho mkuu wa kituo hicho cha Daily Bread Life Tanzania Askofu Mchungaji Mpeli Mwaisumbe amesema imekuwa ni kawaida ya kituo hicho kukaa pamoja na watoto hao kula nao chakula na kuwa kila mwaka wamekuwa wakifanya hivyo .
Alisema kuwa pamoja na kituo kutekeleza jukumu lake la kusaidia malezi ya watoto hao wadau mbali mbali wamekuwa wakiunga mkono jitihada za kusaidia watoto hao akiwemo Geofrey Mungai ambae ni mkandarasi mkubwa Iringa na mkurugenzi wa Hoteli ya Mount Rayol Villa ya mjini Iringa ,wanasiasa na na viongozi wa serikali na wengine .
Askofu Mwaisumbe alisema kuwa kituo chake cha DBL kilichopo chini ya usimamizi wa mchungaji Neema Mwaisumbe kina zaidi ya watoto yatima 40 na kuwa maendeleo ya kituo hicho yametokana na jitihada za wadau mbali mbali ambao wameendelea kujitolea kusaidia kituo hicho.
Wakati huo huo Askofu Mpeli alitoa rai kwa watendaji wa kituo hicho kuendelea kufanya kazi kwa kushikamana kwa kuheshimu wito walioitiwa na Mungu na kuendelea kuwalea watoto kwa Upendo kwa Mwaka ujao wa 2022.
Aidha alisema kuwa wadau wanaoendelea kusaidia kituo hicho ni wengi zaidi na kuwa kwa umoja wao kituo hicho kinaendelea kuthamini michango yao na kuomba kuzidi kujitolea zaidi kwa ajili ya watoto hao kwa ajili ya kuona watoto hao wanapata elimu Kituo hicho ambacho kina zaidi ya miaka 15 15 toka kuanzishwa kwake kimefanikiwa kuanzisha shule yake ya Sekondari iliyopo kijiji cha Mgera ambayo inapokea na watoto wengine kwa kuchangia ada ndogo zaidi kuzindua shule ya sekondari .
kama umeguswa na jitihada za wale wote wanaojitolea kusaidia yatima wa kituo hiki cha DBL mkimbizi Iringa unaombwa kuchangia mchango wako wowote kupitia namba hii ya mkurugenzi mtendaji wa kituo hiki mchungaji Mpeli kupitia huduma ya TIGO PESA 0719239936 na M-PESA ni 0754362536 na Mungu atakubariki na kukuongezea pale ulipopunguza.
Wageni mbali mbali walioshirikia chakula na yatima wa DBL
Mchungaji Neema Mpeli akitoa neno





0 Comments