Header Ads Widget

KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2022 KUFANYIKA KAGERA

 





Kilele cha  mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2022 zinatemegewa kufanyikia mkoani mkoani Kagera huku wananchi wa mkoa huo hasa wafanya biashara wakihaswa kutumia frusa hiyo kujipatia kipato...Na, Titus Mwombeki-MTDTV BUKOBA.


Hayo yamesemwa na katibu tawala wa mkoa wa Kagera prf. Faustine Kamuzola akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge katika mkutano mkuu wa jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania (JWT) mkoa wa Kagera ulioambatana na uchafuguzi wa viongozi wa chama hicho shuli iliyofanyika katika ukumbi wa ELCT Hotel uliopo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.


“Tutakuwa na ugeni mkubwa katika mkoa wetu wa kagera, kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru zitafanyikia hapa kwahiyo ni frusa kwa wafanyabiashara wote walioko mkoani kagera kutumia muda huu kuanza kujipanga hasa  kuboresha huduma zenu kwani nyie ndio watoa huduma na hii itawasaidia kujiingizia kipato”



Aidha amewataka viongozoji katika mkoa huo kuwaruhusu  wanyabiashara kufanya bishara zao muda wowote wanaoutaka kama hakakuna viashiria vya uvunjifu wa amani.


“Duniani kote siku inasaa 24 sisi Tanzania tunadhani muda wa usiku nimuda wakulala lakini wenzetu kuna ambao uchumi unafanya kazi saa24 sasa, sasa wenzako wanafanya kazi saa24 na wewe unafanya saa12 unategemea unaweza kujilinganisha nao? Mkurugenzi na mstahiki meya mlioko hapa tafadhari kama biashara inaweza kufanyika saa24 waacheni watu wakafanye hasa kama hakuna viashiria vya uvunjifu wa Amani”



Naye makamu mwenyekiti wa umoja huo Bi.Samira Khalfani awakati akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa na wafanyabiashara wa mkoa huo kuwa makamu mwenyekiti, amewataka wafanyabiashara hao kushikamana kwani itawasaidia kutatua changamoto mbalimbali.


“Tatizo la wafanya biashara wa mkoa huu hatupendani ndiyo maana hatuendelei, sasa niwaombe kuanzia sasa tushirikiane, tujumuike pamija na tupendane, frusa ni nyingi na tuache uvivu”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI