Header Ads Widget

ELIMU YA KUJIAJIRI YATOLEWA KWA VIJANA MKOANI KILIMANJARO


Vijana  Nchini wametakiwa kutosubiri nafasi za  Ajira pale wanapohitimu masomo yao na badala yake wajiajiri wenyewe Kwa kufanya bishara ili  kuwaajiri wengine na kupunguza changamoto ya Ajira iliyopo hapa  nchini.Mwandishi  Rehema Abraham ,MDTV KILIMANJARO


Kauli hiyo imetolewa November 30,2021 na Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la Kiserikali  la Asante Afrika Foundation  lililopo Jijini Arusha  Theopista Seuya wakati alipokuwa  katika mafunzo ya kuwapa ujuzi na uelewa vijana  waliopo mashuleni na wa Elimu ya Vyuo yaliyofanyika Mkoani Kilimanjaro.


Aidha amesema kuwa  shirika hilo la Asante Afrika limejikita katika kuwapa vijana  Elimu kuanzia ngazi ya shule za msingi hadi  vyuo  ambayo itawasaidia vijana vijana wengi ambao  wamemaliza vyuo vikuu na hawajajiriwa na wapo mitaani  kisubiri Ajira kuweza kujiari wenyewe .


"Tunatamani vijana wapate ujuzi ambao utawasaidia mara baada ya kumaliza shule na hilo ndio lengo la shirika la Asante Afrika Foundation ,tunataka vijana waweze kuishi maisha bora hata baada ya kumaliza masomo wawewameajiriwa au hawajajiriwa waweze kujitegemea wenyewe.


Tokana na mabadiliko yaaliyopo katika jamii vijana wanapaswa kubadilika ili kuendana na wakati Kwa kuwa wabunifu ,na kupata ujuzi na maarifa yanayoendana na changamoto zilipo ili kuweza kukabiliana nazo.



Meneja wa mradi wa yourth livelihood program Glory Mushi kutoka katika shirika hilo amesema kuwa mafunzo hayo yamewakutanisha   vijana 65 kutoka mikoa mitatu ambayo ni Arusha , Kilimanjaro, Tanga.ambapo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia ujuzi ,maarifa,na nyenzo za kuweza kukuza biashara zao.

"Ukosefu wa Ajira kwa Tanzania upo kwan vijana wengi wamekuwa wakimaliza vyuo na kukosa Ajira hivyo shirika hili linafanya kazi ya kuwapatia vijana ujuzi ili waweze kukabiliana na changamoto hiyo  ya Ajira na waweze kuja na maarifa yenye ubunifu "Alisema Glory.

"Tunawaanda kwanza kisaikolojia wakiwa shule za awali ili wajue kuwa sio tu mpaka wamalize chuo wasubiri Ajira Bali waanze kujiajiri kabla ya kuhitimu masomo yao"Alisema Glory.


Hata hivyo mafunzo hayo yanatolewa na shirika hilo kwa vijana ambao hawana uwezo na ambao hawafikiwi ,Kama maeneo ya vijijini .



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS