Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu, amesema ameridhishwa na ujenzi wa kumbi pacha za hostel ya wasichana ziara katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru(TICD) Mkoani Arusha.
Dkt. Jingu ameyasema hayo akikagua maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo katika ziara yake chuoni hapo leo tarehe Desemba 17, 2021.
Aidha, Dkt. Jingu amepongeza hatua ya chuo ya kuamua kujenga kituo cha Kitaifa cha ubunifu na uendeshaji kwa ujumla ambapo ameahidi kuwa Wizara itaunga mkono jitihada za ujenzi wa mradi huo.
Amesema amefarijika na jitihada zinazofanywa na uongozi kwa kusimamia kikamilifu ujenzi huo. na kuagiza mradi ya ujenzi wa kumbi pacha za mihadhara kukamilika ifikapo Februari 14, 2022 na hosteli ya wasichana kukamilika ifikapo Aprili 30, 2022.
Mapema akisoma taarifa ya ujenzi huo, Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Bakari George, alibainisha kuwa Taasisi imenunua eneo la ekari 4.1 eneo la Nambala (Halmashauri ya Wilaya Meru) kwa ajili ya kujenga kituo cha Kitaifa cha Ubunifu na kumbi ndogo za Mihadhara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa miradi hiyo John King Gwanyemba ameahidi kukamilika kwa miradi hiyo kadri ilivyoagizwa na Katibu Mkuu.





0 Comments