Header Ads Widget

CHAPUO LA ELIMU YA ZIADA. V

 



Kulingana waraka nambari 3 wa mwaka 2016 wa utoaji wa elimu ya msingi bila malipo umeyataja majukumu ya Wizara ya Elimu na TAMISEMI na kuzipachikia majukumu ambayo kwa jumla ni majukumu 13, majukumu sita kwa Wizara ya Elimu na saba ya TAMISEMI........NA ADELADIUS MAKWEGA _MBAGALA.


Kwa upande wa TAMISEMI kwa mujibu wa waraka huu wa elimu bure wao wanamajukumu saba kama nilivyokwambia. Jukumu lake la kwanza ni kufanya tafsiri ya nyaraka hizo. Binafsi naona ni jukumu la kawaida sana ambalo nadhani wala halikupaswa kutajwa katika waraka huu, kwa kuwa nyaraka hizo ni za kisomi na wanapatiwa ni wasomi na zinaeleweka.


Jukumu la pili ni kutoa mwongozo wa matumizi ya fedha za umma ambapo hapa ni kuandika barua ambayo ni kazi ya kitarishi ambayo nadhani kuelekeza matumizi ya fedha hizo zilizotengwa kubwa ni kuhakikisha matumzi sahihi tu.


Jukumu la tatu ni kutoa mwongozo wa matumizi ya fedha za umma kwa wakuu wa shule hilo halina shida ni mojawapo ya majukumu yake kwa kuwa TAMISEMI ndiyo yenye shule. Hapo ushauri ni kwa kuwa uteuzi wa wakuu wa shule ufanywe na wilayani na siyo mkoani, mkoa hauna shule bali wilaya ndizo zenye shule na nia ni kuwa matokeo chanya.Hoja ya kuwajibishana itakuwepo wilayani.


Jukumu la nne ni la kuratibu na kuandaa mipango ya bajeti ya kila mwaka juu ya elimu bure ambao hili wanachofanya ni kupata bajeti ya kila kila shule, kila wilaya na kila mkoa nia na kuzijumuisha pamoja ilikupatikana bajeti ya jumla ya pesa ya elimu bure zitakazoombwa kulinga na mgao wa bajeti kwa mwaka huo.


Tano ni kufanya ukaguzi kuwa kama hiyo elimu bure inavyotolewa. Kumbuka pia kazi hii inafanywa na wadhibiti ubora wa elimu pia ni kazi sahihi kwa TAMISEMI sasa inapaswa kuongezewa nguvu kwa hawa Wadhibiti ubora wa elimu kuwa TAMISEMI.


Jukumu la sita ni kutoa taarifa za hali ya elimu bure kwa Wizara ya Elimu. Utoaji wa taarifa kutoka kwa wizara kwenda nyingine, nadhani siyo sahihi, kwani wizara zote zinawajibika kwa Rais. Chini ya ufuatiliaji wa karibu kwa Waziri Mkuu,kwa kuwa TAMISEMI sasa kama nilivyopendekeza ndiyo itakayosimamia elimu tangu awali hadi kidato cha sita hilo litakufa.


Saba na mwisho ni utengaji wa fedha zitakazotumika katika kuendesha shule. Hapa ndipo kwenye ngoma lazima pesa zitolewe za kutosha kulingana mahitaji ya jamii. Hapo panaweza kutengwa pesa na kuonekana zimetengwa tu na zikifika pesa hizo haziwezi kufanya lolote lile. Jambo hilo ndilo linaloleta mashaka makubwa na malalamiko.


Katika majukwaa ya siasa inasemwa kuwa elimu ni bure lakini hiyo pesa inayotolewa inatoshwa? Hapa ukiziuliza Bodi/Kamati za shule wanayajua mengi juu ya kiasi cha fedha hizo kama zinatosha au laa. Jibu lake pesa hizo ni kidogo sana, walimu wakuu huwa wanazikusanya baada ya miezi mitatu au minne ndiyo wanapata pesa ya kufanyia kazi ndogo kama kununua vifaa vya kufundishia kama chaki..


Shida kubwa ambayo ndiyo inaonekana sasa haswa ni viongozi wa kisiasa wanatoa matamko ya elimu bure na pesa inakwenda. Lakini kumbuka kuwa Wenyeviti wa Bodi/Kamati za shule ndiyo wanazozisimamia pesa hizo wanaona kila kitu na siyo siri wanatambua ukweli.Hata ukirejea majukumu ya bodi/kamati hizi za shule kwa mujibu wa waraka nambari 3, 2016 wa elimu bure unasema wazi.


Hoja ya leo ni kuwa pata picha ya idadi ya shule za umma nchini, kumbuka kila shule ina wajumbe wa bodi/kamati zikiwa chini ya Mwenyekiti na katibu wake akiwam ni mkuu wa shule iwe ya sekondari/msingi. Hawa wote bila ya kujali mitazamo yao ya kisiasa iwe CCM au CHADEMA wanatambua kuwa pesa inayotolewa kama inatosha au haitoshi, kila mwenyekiti na bodi /kamati wanalo jibu.


Hawa wajumbe wa Bodi/Kamati za shule wanakutana na wazazi/walezi katika vikao vya shule na kuwaeleza ukweli. Kumbuka nilieleza kuwa Wenyeviti wengi wa Bodi/Kamati za shule huwa wengi ni watu waadilifu/waliotumikia nchi yetu kwa ngazi mbalimbali na wengi ni watu wa ibada san asana iwe msikitini/kanisani, hawana ndimi mbili.


“Jamani wazazi mmemsikia mkuu wa shule ambaye ni katibu wa Bodi ya shule yetu ambaye ni katibu wangu amesoma kiasi cha fedha kilicholetwa kwa miezi mitatu iliyopita kwa hiyo pesa hii imetumika kuwekea ubao wa kufundishia katika darasa lile jipya tulilojenga, sasa tuna shida ya mwalimu Physics kwa kidato cha nne tunafanyaje.”Mwenyekiti bodi anasema.


Mwenyekiti wa bodi anaweza akawa tayari ameshafanya utafiti wa gharama za kumlipa mwalimu huyo ziada kwa mwezi wa 12 na atakubaliana kuwa sasa kila mzazi mwenye mtoto katika dasara hilo kutoa kiasi fulani hili somo hilo kufundishwa. Vinginevyo mtihani ukija watoto wao watakula wa chuya. 


Haya ni mambo ya kawaida kwa sasa unapoyapiga marufuku inaleta mtazamo ambao siyo mzuri kwani hili linalofanyika siyo jambo baya. Naweka kalamu yangu chini kwa siku ya leo kwa kusema kuwa Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako na Mheshimiwa Ummy Mwalimu katika kulisemea suala la masomo ya ziada mnatakiwa kuwa makini mno.


makwadeladius@gmail.com

0717649257

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI