Header Ads Widget

BEKI WA ARSENAL GABRIEL MAGALHAES APAMBANA NA MWIZI ALIYETAKA KUIBA GARI LAKE

 


Maelezo ya video,

Kanda ya Video ya CCTV ilimuonesha beki huyo akipigana na mwizi huyo aliyejaribu kumuibia gari lake

Nyota wa ligi ya Premia Gabriel alikabiliana na mwizi aliyebeba rungu la mchezo wa baseball ambaye alijaribu kuiba gari lake.

Beki huyo wa Arsenal alifuatwa nyuma hadi nyumbani kwake eneo la Barnet London na watu watatu tarehe 20 Agosti waliomtaka kuwapatia funguo zake za gari lake.

Kanda ya video ya tukio hilo inamuonesha Gabriel kijaribu kukabiliana na mtu aliyebeba rungu la mchezo wa baseball ambaye baadaye alijulikana kama Abdi Muse.

Muse mwenye umri wa miaka 26 alihukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa makosa ya wizi wa mabavu katika mahakama ya Harrow Crown mnamo tarehe 17 Novemba.

Baada ya kuzidiwa nguvu mwizi huyo alitoroka na funguo za gari la Gabriel lakini akaliwacha gari hilo nyuma katika gereji.

Baadaye jamaa huyo alikamatwa na maafisa wa polisi na kushtakiwa na wizi wa mabavu na kumiliki silaha hatari.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI