Header Ads Widget

WAKAZI WA KIJIJI CHA NYANGOVA WAFUNGIWA MITA ZA MAJI ZINASOMA UPEPO BADALA YA MAJI

 


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma akiongea na wakazi wa kijiji cha Nkungwe(hawapo pichani)baada ya kukagua mradi wa maji katika kijiji hicho

Na Editha Karlo,MDTV Kigoma

WAKAZI wa Kijiji cha Nyangova kata ya Nkungwe Wilaya ya Kigoma wamesema kuwa baadhi ya mita za maji walizofungiwa na wakala wa maji mjini na vijijini(RUWASA)  katika maeneo yao zimekuwa zikosoma upepo badala ya maji hali inayopelekea kulipa bili za maji ambazo si sahihi.


Hayo wameyasema leo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenya alipotembelea kwenye mradi wa maji wa kijiji cha Nkungwe sambamba na kusikiliza kero za wananchi wa kijiji hicho.


Wakazi hao walimweleza Mkuu wa Mkoa tatizo hilo la baadhi ya mita zao za maji zilizofungwa kwenye maeneo yao zinasukuma upepo tu badala ya maji kama inavyotarajiwa.


"Huu mradi wa maji ambao serikali imetuletea hapa kijijini kwetu  ni mzuri ila changamoto zipo ikiwemo hii unakuta mita zinazunguka upepo tu badala mita izunge maji yatoke yasome hili kwakweli ni tatizo linatutesa"Alisema Kadomo Hamenya Mkazi wa Kijiji cha Nkungwe.


Wakazi hao waliitaja changamoto nyingine katika mradi huo ni baadhi wamechelewa kuunganishwa kupata huduma ya maji kwa wakati japo taratibu zote za kuunganishiwa maji wamefanya.


"Mimi toka mwezi wa nne mwaka huu nimeomba kuunganishiwa maji nyumbani kwangu nikachimba na mtaro ila hadi leo naona kimya,nyumba yangu inataka kubomokoka sababu ya mtaro nataka nikaufukie tu sababu hauna faida yoyote"alisema Aselini Domeze mkazi wa Kijiji cha Nkungwa.


Awali akisoma taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Meneja wa wakala maji mijini na vijijini(RUWASA)Halmashauri ya Kigoma mhandisi Leo Respicius amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa linatokana na ubovu wa baadhi ya mita za wateja ambapo maji yakifungwa zenyewe huwa zinaendelea kuzunguka tu.


Alisema tayari wameanza kushughulikia tatizo hilo kwa kuruhusu maji kukaa kwenye mabomba muda wote.


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ameiagiza RUWASA kuhakikisha changamoto hiyo inakwisha na wapate huduma ya maji kwa gharama halisi za matumizi yao.


"Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu imadhamiria hadi kufikia mwaka 2025 iwe imekwisha au imepungua kwa kiwango kikubwa,hivo mirado hii ni ya wananchi sisi tunawajibu wa kuilinda ili tusirudi kule tulipotoka"alisema Andengenye

Alisema Rais anataka pesa za kodi ziende kufanya kazi za maendeleo ambayo yanamgusa kila mwananchi kwa kupata huduma bora za kijamii.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma anaendelea na ziara ya kukagua Mkoani humo sambamba na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.



Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Nkungwe wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye(hayupo pichani)wakati akitatia kero zao mbalimbali baada ya kutembelea mradi wa maji katika kijiji hicho

Mhandisi Leo Respicius Meneja wa wakala wa maji mijini na vijijini(RUWASA)Halmashauri ya Kigoma  akisoma taarifa ya mradi kwa Mkuu wa Mkoa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI