Agizo la Waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa la kila kata na kijiji kulima zao la mkonge limeanza kutekelezwa katika Kata ya Ubena kwa wananchi kuanza kulima heka 10 ili kujiongezea kipato binafsi na taifa.
Akizungumzia katika mkutano wa wananchi wa kata ya Ubena katika viwanja vya kijiji cha Visakazi Chalinze mkoani Pwani Diwani wa Kata ya Ubena Jofrey Kamugisha akihamasisha kulima kilimo hicho cha zao la mkonge ambapo amesema kata hiyo imeshatenga jumla ya heka 35 za kulima mkonge katika sehemu tatu tofauti za kata hiyo ya Ubena ili wananchi waanze kunufaika na kilimo hicho cha mkonge.
Alisema kupitia uhamasishaji kwa wananchi ili agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu litekelezwe katika kata hiyo na Kilimo cha mkonge kiweze kuinuliwa na kuleta tija kwa wananchi wameamua kuanzia kilimo hicho kwenye taasisi za serikali na katika shule za msingi na sekondari maana watoto huko ndiko wanajifunza mambo mbalimbali lakini pia wanataka wajifunze kilimo hicho cha mkonge.
"Tunataka hamasa hii iwe na mahali ilipoanzia hivyo ianzie mashuleni wanafunzi washiriki katika kulima na kutunza mashamba hayo ya mkonge lakini wakati wanatunza mkonge huo na wao wanakuwa wakijifunza kwa vitengo namna ya kulima na kutunza zao hilo muhimu la kibiashara ili hata baada ya kuhitimu masomo yao pia wanakuwa wamepata ujuzi katika mashamba hayo darasa".
0 Comments