Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi, Robert Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Wurzburg nchini nchini Ujerumani, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Amina Makilagi pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwaza Sima Costantine
Na Adrian Audax - MDTV MWANZA
Meya wa Jiji la Wurzburg nchini Ujeruman Mheshimiwa Christian Schuchartd amehaidi kuendeleza ushirikiano kati ya Jiji ilo na Jiji la Mwanza,
Ameyasema hayo katika ziara ya kukakuga miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la mwanza kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la Wurzburg ambao umelenga katika sekta ya utalii,
Meya Schuchartd amesema kuwa Jiji la Wurzburg litaendelea kushirikiana kwa ukaribu na Jiji la Mwanza na kuhaidi kuamasisha Uwekezaji kutoka Ujerumani kuja Tanzania,
Naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Robert Gabriel amesema kuwa Mwanza mi kitovu cha utalii hivyo yuko tayari kushughulikia upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa Hoteli kubwa za kisasa, na hivyo kuwataka wawekezaji kutoka Ujerumani wachangamkie fursa hiyo
0 Comments