Header Ads Widget

MUTAFUNGWA AFUNGUKA NA KUWATANGAZIA KIAMA MADEREVA WAVUNJA SHERIA

 .        


SACP Wilbrod Mutafungwa-Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Nchini akigawa vipeperushi kwa Madera na Wadau stendi mpya Makambako.

Na Frederick Siwale - Mdtv Media Njombe.       

KAMANDA wa kikosi cha usalama barabarani Nchini ,Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Wilbrod Mutafungwa amewatangazia kiama madereva wavunja sheria za usalama barabarani kuelekea mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka ujao.                                   


SACP Mutafungwa aliyasema hayo katika Halmashauri ya Mji Makambako Mkoani Njombe wakati wa ziara yake ya kikazi kupitia doria za kikazi wakati akizungumza na madereva wa malori yafanyayo Safari ndefu za kutoka Nchini Tanzania kwenda Nchi jirani za kusini mwa Afrika.          


SACP Mutafungwa alisema Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani Makao makuu kimeamua kutoka nje ya Ofisi kupitia barabara kuu ya Dar es salaam kwenda Mbeya na Kanda yote ya nyanda za juu kusini ,wakati Maafisa wengine wakitokea Dar es salaam kwenda Arusha kwa Kanda yote ya Kaskazini na wengine kutoka Dar es salaam kwenda barabara kuu ya Mwanza kwa Kanda ya Ziwa ili kuona uwezekano wa kupunguza ajali kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka ujao.                                     



Pamoja na doria hiyo SACP Mutafungwa alitoa elimu na kugawa vipeperushi ambavyo vitasaidia Madereva na Wadau wengine kujifunza mambo muhimu yahusuyo usalama barabarani huku vikibeba ujumbe na kauli mbiu isemayo " JALI MAISHA YAKO NA YA WENGINE" 

 

Akizungumza na madereva wa malori na mabasi katika kituo cha mizani Makambako na stendi mpya Makambako SACP Mutafungwa alisema Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani na Wadau wengine wamejipanga kutoa elimu kwa madereva na kwamba wale kichwa ngumu wataonywa na wasiposikia watapunguziwa madaraja kutoka C hadi A1 na ikionekana hawawezi kusikia basi badala ya kuendesha basi au gari kubwa watapewa leseni ya kuendeshea pikipiki tena bila kubeba abiria.                                      


Katika doria hiyo alisema Jumla ya mabasi makubwa yafanyayo Safari zake kutoka Dar es salaam kwenda mikoa ya Kanda ya nyanda za juu kusini madereva wake 26 waliadhibiwa huku mmoja akachukuliwa leseni yake na kutakuwa kuripoti kituo cha Polisi Makao makuu ya kikosi cha usalama barabarani Nchini Jumatatu ya Novemba 15 kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.                                  

Aidha SACP Mutafungwa alisema lengo na madhumuni ya doria hiyo kwa Nchi nzima ni kupambana na kudhibiti ajali kuelekea mwisho wa mwaka huu na mwazo wa mwaka ujao na ikiwezekana Tanzania kipindi chote iwe salama isiyo na ajali za hovyo hovyo.                   




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI