Header Ads Widget

TASAC YAKUTANA NA WADAU MTWARA

 


Na Mwandishi wetu, Mtwara


Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) likishirikiana na baraza la wasafirishaji Tanzania (TSC) na ISCOS wametoa mafunzo kwa wadau wa usafirishaji nchini.


Akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Tasac Kaimu Abdi Mkeyenge ambaye pia ni Meneja Udhibiti wa Huduma za Usafiri kwa Njia ya Maji Fatuma Masenene  amesema kuwa TASAC wanawajibu wa kuwakutanisha na kuwajengea uelewa wasafirishaji.


Alisema kuwa kutokana na matumizi makubwa ya usafairishaji wa shehena kutumia bahari kuwa mkubwa hadi kufikia asilimia 90.


“kwa niaba ya serikali tunamani kuona mnazifahamu mbinu mbalimbali ili muendane na maendeleo na mabadiliko ya kibiashara nchini uwezo wa usafirisjhaji ni jambo muhimu kwao”


Mafunzo haya yatawafanya wajiamini na itawapa nafasi ya kufanyakazi kubwa ya kudhibiti na kusaidia wasafirishaji ili wawe na uwezo mkubwa wa kufanyakazi kwa weredi bila kuathiri usafirishaji majini nchini”


Iscoss imetenga bajeti ya kuweza kuwajengea uwezo hawa wasafirishaji ni jambo kubwa tunaliona kwa ukubwa zaidi tunaziona kazi kubwa za bandari ni kupakua na kupakia tu hivyo ufanisi wa wasafirishji ni jambo la muhimu zaidi”


Serikali imelenga kuwasaidia wasafirishaji majini ni muhimu wakati ambao TASAC ina ratibu namba ya kutekeleza wajibu wake kisheria kwakuwatambua wasafirishaji” alisema Masenene


Nae Katibu mtendaji wa baraza la wasafirishji shehena nchini Salu Johnson alisema kuwa usafirishaji wa shehena nchini zimekwama.


“Kutokana na kukwama kwa usafirishaji wa shehena za makasha tunaangalia meli ambazo zilisimama kufanya kazi zamani Conversion Cargo” alisema Johnson  


Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya intergovernmental standing committee on shipping (ISCOS) Omary Mzuzuri  alisema kuwa jitihada kubwa ziliwekwa ili kuhakikisha kuwa bandari ya mtwara inatumika kwa usafirishaji wa korosho.


“Zipo jitihada kubwa zinafanyika ili bandari ya mtwara iweze kutumika tatizo ni makasha kukwama nchi za marekani na china ambapo mizigo haijashushwa na kusababisha makasha kuwa adimu hii kwetu” alisema Mzuzuri


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI