Header Ads Widget

TANROAD WAFIKISHA ELIMU KWA UMMA JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA BARABARA KWA WATUMIAJI

 



Katika wiki ya nenda kwa usalama barabarani,wakala wa barabara Tanzania(Tanroad) wameendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya  utunzaji wa miundombinu ya madaraja ,viwanja vya ndege na miradi mingine wanayoitekeleza.


Akizungumza baada ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani,Mkuu wa usalama barabarani na mazingira kutoka Tanroad makao makuu,Zapharan Madai alisema Tanroad wameshiriki kikamilifu katika zoezi la utoaji elimu kwa wananchi juu ya kazi  wanazofanya katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya barabara.


"Lakini vilevile tumejikita kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya hizo barabara wanazozojenga hivyo tumekuja na njia mbalimbali za utoaji elimu ikiwemo kwa njia ya vipeperushi ambavyo huwapa wananchi ili wanaposoma waweze kupitia na kufahamu barabara zinazojengwa na Tanroad ikiwemo barabara ya mzunguko iliyopo jijini Dodoma,"alisema Mkuu huyo.


Alisema pia kupitia maonyesho hayo wananchi watapata kufahamu miradi wanayoitekeleza Tanroad pamoja na mradi wa rusaunga rusumo na  barabara ambayo inajengwa kwa kiwango cha zege inayoitwa rusitu mawengi ipo mkoani Njombe inatakribani kilometa 50.



Pia alisema wanayo miradi ya mikakati ambayo ni pamoja na daraja la Tanzanite linaloendelea kumaliziwa pamoja na barabara zake za kuingilia.


Madai alisema vilevile wanao mradi wa kigongo busisi unaoendelea pamoja na miradi mingine iliyokwisha kukamilika ya kimakakati hivyo wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi mambo mbalimbali ya barabara kwani kuna mazingira ya barabara ambayo inajumuhisha pembezoni ambapo kuna misitu,uoto wa aina mbalimbali na vinginevyo.


"Haya ni mazingira ya barabara yanayofaa kutunzwa kwani kwa kutokufanya hivyo ni moja ya kuharibika kwa miundombinu ya barabara kama ilivyopangwa,"alisema 


Madi alisema kupitia mfano hai wa barabara  katika maadhimisho hayo wanaoonyesha wananchi pamoja na alama zote iliyosheheni uoto wa asili,hifadhi ya barabara ,wanyama pamoja na njia za wapita kwa miguu lengo ni kuonyesha usalama wa mtu kupita barabarani pamoja na waendesha vyombo vya moto katika eneo la barabara.



"Barabara zetu zinahifadhi zilizotengwa kabisa katika barabara kuu na mikoa tunazozihudumiani jumla ya mita 45 ikiwa kushoto ni mita 22 na nusu na kulia ni mita 22 na nusu isipokuwa katika maeneo maalumu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI