Afisa Tarafa wa Mihambwe Emmanuel Shilatu Novemba 8, 2021 aliendelea na ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi.
Gavana Shilatu alitembelea miradi ya ujenzi ya kituo cha Afya cha Tarafa ya Mihambwe, vyumba vya Madarasa shule za Sekondari na shule shikizi inayooendelea kujengwa ndani ya Tarafa ya Mihambwe na huku akisisitiza kasi ya ujenzi iongezwe huku ubora na viwango vinavyoendana na thamani ya fedha ya mradi husika uzingatiwe.
"Tarafa ya Mihambwe tulisha puliza kipyenga cha ujenzi. Nahitaji kuona kasi, ubora na viwango vikizingatiwa kwenye miradi yote ya kimaendeleo. Tunataka ifikapo mwishoni wa mwezi huu Novemba ndani ya Tarafa ya Mihambwe tumkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kazi aliyotutuma ya ujenzi huu ikiwa imekamilika vyema. Kwahiyo tujitume vilivyo ikamilike kwa wakati." Alisisitiza Gavana Shilatu.
Tarafa ya Mihambwe imepata fedha Tsh. Milioni 250 (Tsh. 250,000,000/=) za tozo ya miamala ya simu za kujenga kituo cha Afya Mihambwe na Tsh. Milioni 420 (Tsh. 420,000,000/=) kujenga Madarasa 21 fedha za mkopo nafuu za kupambana na Uviko 19 kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Taifa.
0 Comments