Header Ads Widget

SERIKALI YAFUNGUA MILANGO MAKAMPUNI BINAFSI KUAGIZA MBOLEA

 


Serikali imefungua rasmi milango kwa makampuni binafsi kuingiza mbolea nchini na kuwauzia wakulima kwa bei nafuu.

Waziri wa kilimo profesa Adolf Mkenda amesema serikali itahakikisha bei ya mbolea inapungua, na kutoa rai kwa makampuni binafsi kushirikiana na serikali kukabiliana na changamoto hiyo.


Akizungumza leo mkoani Iringa  wakati wa zoezi ugawaji wa mbolea kwa wakulima wa kijiji cha ugwachanya Wilayani Iringa lililoandaliwa na shirika la one acre  fund,

``tunaingia kazini, tumeingia kazini Tunaamini bei ya mbolea itapungua makampuni binafsi tunawakaribisha  tuendelee kufanya kazi tusitafute faida kubwa katika kipindi hiki tushikane mkono wote tujaribu kumiakidogo kidogo ,,

Aidha Waziri prof.Mkenda amepongeza utaratibu wa kukopesha mbolea kwa wakulima kwa gharama nafuu uliofanywa na shirika la one acre fund ,na kuyataka mashirika mengine kuiga mfano huo.

``Nawashukuru sana onea cre fund kwasababu nyie si kwamba tu mmeleta mbolea nyie mmetengeneza utaratibu wakuhakikisha mkulima anaipata mbolea kwa wakati halafu atailipa kidogo kidogo mbele ya safari walau sasa mtu umeshavuna changamoto za fedha unalipa kidogo kidogo na nawahimiza wakulima mnaoingia katika utaratibu huu mhakikishe kwamba mnalipa ili uendelee,,


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Queen sendiga amewataka wakulima kuwaunga mkono one acre fund kwa kulipa mbolea izo kwa wakati ili kuwezesha zoezi hilo kuwa endelevu na kufikia maeneo mengi zaidi ya mkoa wa Iringa.

``Wenzetu wa one acre fund wameleta mbolea na pembejeo kwaajili yetu sisi lakini asilimia kubwa ya pembejeo wanazotupatia wanatupatia kwa mkopo ili tulime tuweze tupata ma zao tuuze na kisha turejeshe fedha ili mfiko huu uendelee kuzungusha na msimu ujao tuweze kupata tena mbolea bila tatizo lolote naomba tuunge mkono one acre fund ili waweze kutusaidia,,

Nao baadhi ya wakulima wa kijiji cha Ugwachanya walionufaika na mbolea hizo kutoka shirika la one acre fund, wamesema kutokana na bei ya mbolea kupanda maradufu,wakulima wengi walipoteza matumaini ya kilimo lakini ujio wa one acre fund umekuwa mkombozi wao..
















 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI