Serikali imeahidi kupeleka fedha zaidi milioni 500 wilaya ya Mwanga kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya Mwanga ili kitatua changamoto ya huduma za afya ukanda wa tambarare.Mwandishi wa Matukio Daima Gift Mongi anaripoti toka Kilimanjaro
Waziri wa nchi , Ofisi ya rais tawala za Mikoa na serikali za mitaa ( TAMISEMI) Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro katika zaiara yake kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa inayotekelezwa kwa fedha kutoka mfuko wa UVIKO 19.
Waziri Ummy amesema Serikali italeta fedha shilingi million 500 kwa ajili ya kujenga majengo matatu kwa kuanzi ikiwemo jengo la mama na mtoto, maabara na jengo upasuaji na jengo la huduma ya wagonjwa wa nje.
"Nimeridhishwa na miradi yenu mmefanya vizuri endeleeni kusimamia miradi ili kwa kuzingatia ubora kulingana na fedha zinazotolewa na serikali ya mama Samia Suluhu,"amesema.
Awali akizungumza mbunge wa jimbo la Mwanga Joseph Tadayo amesema kuwa ujenzi wa hospitali ya ni moja ya ahadi ya rais wakati kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 na kwamba tayari eneo lenye ukubwa wa ekari zaidi 54 zimekwisha tengwa.
Amesema kuwa eneo hilo litatumika kwa ujenzi mradi wa hospitali ya wilaya pamoja na mradi wa chuo cha uganga na uuguzi na kwamba mradi huo utafungua fursa mbalimbali za kiuchumi.
Mkuu wa wilaya ya Mwanga Abdhalah Mwaipaya amesema kuwa hali ya ulinzi na usalama nzuri na kwamba halmashauri ya hiyo imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.





0 Comments