Serikali inatarajia kuanzisha vituo vinne vya umahiri nchini ili vijana waweze kupata ujuzi kwa njia ya vitendo zaidi kwa lengo la kujiajiri kupitia Mradi EASTTIP unaogharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 70 anaripoti Teddy Kilanga kutoka Arusha
Akizungumza katika chuo cha ufundi Arusha walipotembelea mradi unaotekelezwa na fedha za benki ya dunia ,Mkurugenzi wa elimu ya ufundi na mafunzo stadi,Dkt .Noel Mbonde alisema mradi huo unaotekelezwa kupitia fedha zilizotolewa na benki ya dunia kwa lengo la kuanzisha vituo hivyo vya umahiri ikiwemo chuo cha teknolonia Dar es salaam kama kituo cha ICT katika mambo ya Tehama.
"Kituo kingine ni chuo cha ufundi Arusha kama kituo mahiri cha nishati jadidifu lakini pia kuna center nyingine mkoani Mwanza ambacho kitakuwa kwa ajili ya mazao ya ngozi pamoja na na chuo cha usafirishaji(NIT) chenyewe kitakuwa upande wa usafiri wa anga,"alisema Dkt.Mbonde.
Dkt.Mbonde alisema lengo ni kuhakikisha vijana wa kitanzania wanapata elimu itakayowawezesha kupata ujuzi ili waweze kujiajiri na sio kuajiriwa kwani pasipo kumwezesha kijana kupata elimu ya vitendo hataweza kujiajiri.
Alisema vituo hivyo vitakapokamilika wataweza kuzalisha vijana wengi sana wenye ujuzi ikiwa mradi huo unagharimu takribani milioni 75 dola za kimarekani ambapo kwa vyuo vitatu ikiwemo ATC,DIT ya tawi la Dar es salaam na Mwanza kila moja kitapata milioni 16.25 fedha za marekani.
"Lakini kwa upande wa chuo cha NIT kitapata milioni 21.25 dola za kimarekani ikiwa mradi upo katika hatua ya awali ya manunuzi ya vifaa vya ufundishaji katika uendeshaji wake na tunaelekea kwenye maandalizi ya ujenzi na asilimia 80 ya fedha hizi zinakwenda kwenye ujenzi wa madarasa,hostel pamoja na makarakana,"alisema.
Mkurugenzi huyo alisema yaweza kuchukua muda kidogo katika utekelezaji wake ikiwa mradi huo umejikita kwenye manunuzi ya kimataifa katika kufuata sheria za kimataifa na benki ya dunia pamoja na sheria za ndani ya nchi.
Aidha alitoa rahi kwa wasimamizi wa mradi katika kuhakikisha matumizi ya fedha yanaendana na thamani yake.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha,Musa Chacha alisema baada ya kupata fedha hiyo kazi iliyopo ni kusimamia ujenzi wa kituo hicho jadidifu ambacho kitakuwa wilayani hai katika eneo la kikuletwa ikiwa hadi sasa wameshanunia vifaa mbalimbali ikiwemo magari.
Vilele alisema hatua za ujenzi ndio zimeanza katika upatikanaji wa msimamizi wa ujenzi ambaye ni msimamizi wa mradi na baada ya muda ataanza kubuni namna ya majengo yatakavyokuwa ili kuanza kwa ujenzi.
"Tunaamini kuwa hadi kufikia mwaka 2022 katikati tutakuwa tumeshamaliza na wanafunzi wataanza masomo yao na mradi huu umeweka chuo chetu katika misingi mizuri hivyo tunashukuru sana serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kukiwezesha chuo chetu na wizara mama kusimamia vyema,"alisema Kaimu Mkuu wa chuo huyo.
Nae kiongozi mtaalamu wa elimu Kutoka banki ya duniani Xiaoyan Liang alisema wapo Katika kusimamia maono ya usimamizi ya mradi huo Katika chuo Cha ufundi Arusha kwa kusaidia sera ya viwanda ya Tanzania.
0 Comments