Header Ads Widget

MJI KIBAHA KUPATA TSH MILIONI 940 KWA AJILI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde aliyevaa shati jeupe la mikono mirefu alipokuwa kwenye ziara kutembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye baadhi ya shule za Halmashauri hiyo



KUFUATIA Halmashauri ya Mji Kibaha kupata kiasi cha shilingi milioni 940 kwa ajili ya ujenzi wa  vyumba vya Madarasa 47 pamoja na Madawati Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mhandisi Mshamu Munde ametaka ujenzi huo ufanyike usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi kwa wakati. 

Munde ametoa maagizo hayo Mjini Kibaha wakati akipitia maeneo ambayo vyumba vya Madarasa vinajengwa kwa fedha aliyotoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikiwa ni Mkopo kutoa IMF na ni sehemu ya kukabiliana na UVIKO-19.

Amewataka viongozi na wajenzi kuhakikisha kazi inafanyika usiku na Mchana ili ifikapo tarehe 5 Disemba 2021 Madarasa yote yawe yamekamilika tena kwa viwango na ubora unaotakiwa ili kukabiliana ongezeko kubwa la Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2022.

Akiwa shule ya sekondari Simbani pamoja na mambo mengine amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi huo na kwamba ametoa maelekezo ya jumla kuhakikisha kila shule inakamilisha kwa wakati.

Aidha ameshangazwa kuona kamati za manunuzi hazijafanya mchakato wa madawati ilihali fedha zilitolewa siku moja na kwamba kitendo hicho ni kiashiria cha kuchelewesha mradi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI