Header Ads Widget

RUWASA MUSOMA WAJIPANGA KUTOA HUDUMA YA MAJI

Na Shomari Binda MDTV Musoma

WAKALA wa Maji avijijini ( Ruwasa) wilaya ya Musoma  imesema kazi ya miradi mbalimbali inaendelea kuhakikisha wananchi wanapata maji.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kijiji Cha Wanyere Kata ya Suguti,meneja wa Ruwasa,Edward Sironga,amesema yapo maeneo ambayo mabomba yanapita barabarani ilu kufikusha maji kwa wananchi na tayari wamewasiluana na Tanroads ili kupitisha mabomba.

Alisema Kata ya Suguti kuna mradi wa maji ikiwa ni kuwafikishia wananchi majumbani lakini yapo maeneo ambayo hayajapata kutokana na changamoto ya kupitisha barabarani.

Sironga alisema wameshaandika barua Tanroads kuhusiana na hilo na litakapokamilushwa kazi zitaendelea.

" Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suruhu Hassan, tumepewa zaidi ya bilioni 8 kutekeleza miradi ya maji.

' Tunashukuru pia mbunge wa jimbo la Musoma vijijini,Profesa Sospeter Muhongo,kwa jitihada zake za kuwafikishia wananchi huduma",amesema Sironga.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Suguti  wameshukuru kwa kufikishiwa huduma ya maji wakati kipindi cha nyuma walifata zaidi ya kilometa 15.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI