Header Ads Widget

COP26: Waziri anayetumia kiti cha magurudumu ashindwa kuhudhuria kikao


m

Waziri wa Israeli amesema kuwa ameshindwa kuhudhuria mkutano wa COP26 siku ya Jumatatu kwa sababu haukuzingatia watu wanaotumia viti vya magurudumu.

Karine Elharrar aliandika kwenye kurasa ya twitter kuwa "Inasikitisha" kuwa Umoja wa Mataifa haujazingatia watu wenye ulemavu katika shughuli kama hiyo.

Afisa wa waziri mkuu wa Israeli Naftali Bennett amesema wamewasilisha malalamiko yao rasmi kwa waandaaji.

Bwana Bennett alisema hataweza kuhudhuria kikao cha Jumanne kama bi Elharrar hataweza kupata namna ya kufika katika kikao, afisa aliongeza kusema.

Balozi wa Uingereza nchini Israel Neil Wigan aliandika kwenye twitter kuomba radhi kwa waziri.

"Tunataka mkutano wa COP ambao haubagui mtu yeyote," aliandika.

Taarifa zilizoripotiwa kuhusu Bi Elharrar katika Channel 12 ya Israel ni kuwa alishindwa kuhudhuria kwenye mkutano kwa kutumia usafiri wa pamoja au kutembea, mifumo ambayo haukuwa rahisi kwa mtu anayetumia kiti cha magurudumu (CHANZO BBC)

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI