Header Ads Widget

RAIS SAMIA AENDELEA NA SIKU YA PILI YA ZIARA YAKE NCHINI MISRI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa msimamizi Mkuu wa mradi wa  ujenzi wa mji mpya wa kiserikali wa New Cairo Administrative City unaoendelea kujengwa Jijini Cairo nchini Misri, alipotembeleleo na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mji huo jana tarehe 11 Novemba 2021.  Rais Samia yupo Nchini Misri akiendelea na ziara yake ya siku ya pili ya Kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri  Abdel Fattah Al Sisi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan, akitembelea Mji mpya wa New Cairo Administrative City Jijini Cairo nchini Misri  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan, akiangalia ramani ya mji mpya wa kiserikali wa New Cairo Administrative City unaoendelea kujengwa Jijini Cairo nchini Misri, alipotembeleleo katika Makumbusho mapya yaliopo katika mji mpya wa Kiserikali Cairo Misri 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Baadhi ya Wafanya Biashara nchini Misri alipokutana nao  Jijini Cairo Misri ambapo aliwaelezea fursa mbalimbali ziliopo Tanzania. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji saini Hati za makubaliano  katika Nyanja ya kukuza Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Dkt. Maduhu Kazi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Uwekezaji na Biashara Huria nchini Misri Dkt. Mohammed Abdul-Wahabi tarehe 11 Novemba 2021 Jijini Cairo 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan, akishuhudia mabadilishano ya Hati za makubaliano  katika Nyanja ya kukuza Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Dkt. Maduhu Kazi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya  Uwekezaji na Biashara Huria nchini Misri Dkt. Mohammed Abdul-Wahabi tarehe 11 Novemba 2021 Jijini Cairo Misri. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan, akiwa picha ya pamoja na Wafanyabiashara wa Misri baada ya kuzungumza na Wafanyabiashara hao tarehe 11 Novemba 2021Jijini Cairo nchini Misri, ambapo aliwaelezea fursa mbalimbali za uwekezaji ziliopo nchini Tanzania.  Rais Samia yupo Nchini Misri akiendelea na ziara yake ya siku ya pili ya Kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri  Abdel Fattah Al Sisi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI