Header Ads Widget

MWANAHARAKATI BIHIMBA ACHANGIA UJENZI WA KANISA LA GOSPEL REVIVAL ASSEMBLIES OF GOD

 Na Mwandishi Wetu.



Mwanaharakati Bihimba Nassoro Mpaya Mkazi wa Kivule  Ilala Jijini Dar Es Salaam Novemba, 28, amehudhuria ibada katika kanisa la GOSPEL REVIVAL ASSEMBLIES OF GOD na kushiriki katika Tafrija fupi ambapo kanisa hilo lilikua likitimiza miaka minne tangu kuanzishwa kwake. Sambamba na Hilo katika Risala iliyokua imeandaliwa kuna changamoto mbalimbali zilizokua zinalikabili kanisa hilo katika utoaji wa huduma za Kimungu ikiwemo Kusuasua kwa ujenzi wa Jengo jipya na la kisasa la kanisa hilo na Baada ya Risala hiyo Bihimba akawa ameahidi kutatua mambo  mbalimbali kama vile Cement, Mabati , Mchanga n.k kupitia hata kwa marafiki zake katika kikundi cha Wafanyabiashara .



Ndugu Bihimba Nassoro Mpaya (Katikati) akisikiliza neno kutoka kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Gospel Revival Assemblies of God Mchungaji Faraja Mwankeja kulia ni Bwana Mogani

' Ndugu zangu mimi ni mtu wa kawaida sana lakini nataka niache alama , na huwa siko tiyari kukaa nyuma pale ambapo naona kabisa kuna suala fulani ambalo naweza kulifanya kutatua jambo fulani, Risala yenu nimeisoma na nimeisikia pia kwahiyo nachopenda kuahidi ni kwamba hayo mambo yote yaliyoorodheshwa sisi tutayatua , panapoitajika simenti mtapatiwa simenti, panapohitajika mchanga mtapapiwa, mabati alikadharika, tunataka tutengeneza uchangamani bila kujali udini, ukabila  au hata mambo mengine yanayoweza kuondosha amani yetu, na hilo ndilo Taifa alilotwachia baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere'.Alimalizia Bwana Bihimba .



Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Faraja Mwankeja alimpongeza Bwana Bihimba kwa Moyo aliouonyesha katika kuuunga mkono kazi ya Mungu na kutoa wito kwa watanzania wengine waige mfano huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS